BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATZ WOTE KWA UCHAGUZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATZ WOTE KWA UCHAGUZI

BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATANZANIA WOTE KWA UCHAGUZI MKUU WA AMANI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon

NA MWANDISHI MAALIM

NEW YORK

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtumia salamu za pongezi Rais Jakaya Mrisho Kikwete na watanzania wote kwa kukamilisha uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani na utulivu.

Katika pongezi hizo, Ban Ki Moon anasema , “ Mhe Rais, niruhusu nitumie fursa hii kuipongeza serikali yako, wananchi wa Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC),kwa kukamilisha uchaguzi mkuu uliokuwa umeandaliwa vizuri na kufanyika katika mazingira ya amani na uwazi”.

Amesema kwa mara nyingine kwa kupitia uchaguzi mkuu uliomalizika, watanzania , vyama vya siasa na viongozi wa vyama hivyo wameonyesha ukomavu mkubwa na utashi wa kudumisha amani na demokrasia.

Aidha katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemhakikishia Rais Jakaya Kikwete na serikali yake ushirikiano usioyumba kutoka kwake.

Na kwamba UN itaendele kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa malengo na maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages