INTERNET EXPLORER YAVAMIWA TENA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

INTERNET EXPLORER YAVAMIWA TENA

 Internet Explorer imevamiwa tena,Microsoft wametoa angalizo kuwa kuna uvamizi huu unaoweza kuwapata wale wanaotumia Internet explorer hivyo imewataka watumiaji wake kuwa makini.

  Msemaji wa Microsoft amesema kuwa uvamizi huwa unaweza kuwashambulia watumiaji wote wanaotumia matoleo ya 6 na 7.Katika uvamizi huu,mtumiaji hupokea e mail inayokuwa na link ya tovuti fulani,ukibonyeza hiyo tovuti basi utapelekwa kwenye website yao ambayo wataangalia(test) je unatumia toleo gani la internet explorer,kama watagundua unatumia toleo lenye matatizo ambalo ni la 6 au 7 basi watakupeleka(redirect) kwenye tovuti yao nyingine ambapo wataingiza code kwenye kopyuta yako bila wewe mwenyewe kujijua na kuweza kuitawala kompyuta bila idhini yako. 

Kutokana na maelezo kwenye blog ya Microsoft,wanafafanua kuwa hili tatizo linaweza kuathiri hata toleo la 8,ila wamesema toleo la 9 lililopo kwenye majaribio halina matatizo.

Habari njema zinakuja kuwa,ingawa toleo la 8 lipo kwenye utata huu lakini kutokana na udhibiti wake wa kiusalama wa asilia,ni ngumu mtu kuweza kushambuliwa,hivyo kama unatumia toleo la 8 basi upo salama ilihali haujafanya mabadiliko yoyote ya kiufundi tokea uiweke hiyo internet explorer toleo la 8

Hivyo timu ya AfroIT inawashauri wanajamii kutumia toleo jipya la 8 au hata la 9 ili kujihakikishia usaalama zaidi.Ili kudownload toleo jipya la Microsoft tembelea hapa.Pia kuwa makini kwa kutofungua link ammbazo hazina kichwa wala miguu.kwa kufanya hizi utaweza kujiweka katika mazingira ya kiusalama.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages