MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Gwau ametoa bima za afya kwa wanawake 400 mkoani hapa ili ziwasaidie kupata matibabu. Gwau alitoa bima hizo jana wakati akihutubia kwenye kongamano la wanawake Mkoa wa Singida lililofanyika Ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma ambapo pamoja na mambo mengine walitafakari siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwa madarakani na mafanikio ya wanawake hapa nchini huku kauli mbiu ikiwa ni ‘Wanawake ni Nguzo ya Maendeleo’ Kazi iendelee.
” Bima hizi ni zawadi ya Afya kutoka katika mfuko wa ofisi
yangu na nijuhudi za kumuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika
kuboresha afya za akina mama kwani bila afya hakuna maendeleo na ili maendeleo
yaje na kufanya kazi kwa bidii ni budi kila mtu kuwa na afya njema, hivyo
nimeamua kugharamia suala la afya kupitia mfuko wa bima wa CHF kwa wanawake
hawa ambao ni sawa na kaya 400 huku wanufaika wakiwa 2400 pamoja na watu wenye
uhitaji maalumu“.alisema Gwau.
Alisema bima hiyo itakuwa
ya watu sita kutoka kwenye kila familia ya wanawake hao 400. Gwau alisema
mwaka huu ameanza na kaya 400 lakini matarajio yake ni kufikisha kaya 1000 na
wanufaika wakiwa zaidi ya 5000 itakuwa vizuri zaidi na anafanya hivyo kuunga
juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwatumikia watanzania katika sekta ya
afya.
Pia Gwau alisema kuanzia kesho atatoa utaratibu kwenda
kwenye halmashauri zao ambako anatoka kila mwanamke kwa ajili ya kujisajili
ambapo wanatakiwa watu sita yaani baba, mama na watoto wanne walio chini ya
umri wa miaka 18.
Gwau alitumia
kongamano hilo kwa ajili ya kuwashukuru wanawake hao kwa kumchagua kwa kura
nyingi na kuwaomba ushirikiano ambapo pia alieleza mipango na mwelekeo wake wa
kazi za maendeleo mkoani Singida.
Alisema ataanza ziara zake za kikazi katika wilaya zote na
kata ili kwa pamoja waweze kutatua kero za wanawake huku vipaumbele vyake
vikiwa ni kuwainua wanawake kiuchumi na kuwapatia elimu na mafunzo mbalimbali
na kuijenga Jumuiya yao ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT)
Alisema katika masuala ya kuwasaidia wanawake atakuwa
akifanya kwa awamu kulingana na atakavyo jaliwa lakini ya kiutendaji yatakuwa
wilayani ambapo aliwaomba wamshike mkono, wamuelekeze, wamshauri na kumkoasoa
lengo likiwa ni kuijenga Singida.
Aidha Gwau aliwaomba wanawake hao kumuunga mkono Rais Samia
Suluhu Hassan akiwa ni mwanamke wa kwanza hapa nchini kushika wadhifa huo
mkubwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambapo alisema kwa umoja wao wanapaswa
kuonesha mshikamano na jinsi walivyo tayari kufanya naye kazi akiwa katika
nafasi hiyo na kumuombea kwa Mungu.
Katika hatua nyingine aliwataka wanawake hao kuchangamkia fursa ya kilimo cha alizeti kwa kuwa ndio zao kubwa la biashara mkoani hapa na Serikali imeweka nguvu ya kulilima kwenye mikoa mitatu ya Singida, Dodoma na Simiyu.
Pia aliwaomba
madiwani wanawake kusimamia na kuwashauri wanawake kuchangamkia mikopo
kutoka katika halmashauri zao kwaajili ya kujiletea maendeleo na kuinua uchumi
wa mwanamke.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba
ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo alimshukuru Gwau kwa kuandaa
kongamano hilo na kuwashukuru wanawake hao kwa kumchagua kuwa mbunge.
Aliwataka wanawake hao kuwa wamoja na kushirikiana kwa kila
jambo sambamba na kuimarisha jumuiya yao ili chama hicho kiendelee kuongoza nchi.
Katika kongamano hilo Gwau aliwaalika wataalamu ambao walitoa mada kuhusu masuala ya afya hususani namna ya kujikinga na ugonjwa wa corona na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)