Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Naibu waziri wa viwanda na biashara Stellah Manyanya wakifungua kitambaa wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
|
|
Waziri wa Viwanda na Biashara,Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara katika hafla ya ukizindua wa kliniki ya Biashara uliofanyika katika maonesho ya kimataifa yanayo fanyika Sabasaba jijini Dar as Salaam.
|
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Azania bank mara baada ya uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
- Ni benki ya kwanza ya kiasili inyowezesha huduma zote za kifedha sehemu moja kwenye Kliniki ya Biashara iliyopo kwenye maonyesho ya Sabasaba
Dar es Salaam, Julai 3, 2018: Benki ya Azania (ABL) ambayo ni benki binafsi ya kiasili hapa nchini, imeelezea nia yake ya kuendelea kusaidia sekta mbali mbali za kiuchumi kwa kutoa huduma mahususi za kifedha hususani katika kipindi hiki cha maonyeshao ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Charles Itembe alisema lengo la benki hiyo ni kutoa huduma za kifedha kwa wazalishaji bidhaa, viwanda pamoja wakulima kwa ajili ya kusaidia kukuza biashara zao.
Kliniki hiyo ambayo itatoa huduma zote za ushauri wa masuala ya kibiashara sehemu moja, imeundwa na mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE)
Ikiwa na kauli mbiu “Kusaidia Maendeleo Endelevu na ukuaji wa Biashara”, Kliniki hiyo itakuwa ni ya kwanza na ya aina yake ambayo itatoa ushauri kwa aina mbali mbali za biashara ikiwa ni pamoja na biashara ndogo, za kati na kubwa ambazo zitakuwa zinashirikim katika maonyesho ya Sabasaba
Mkurugenzi huyo alisema benki ya Azania inatoa huduma mbali mbali za kifedha ikiwa ni pamoja na mikopo ya biashara, mikopo binafsi, mikopo ya nyumba na mikopo hiyo hutolewa kwa riba ndogo
“Tunawakaribisha watu wote wanaoshiriki maonyesho ya Sabasaba na wanaokuja kutembea kwenye banda letu kwa ajili ya kupata huduma zan kifedha,” alisema
Alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ni pamoja na kusaidia bishara za kuuza bidhaa nje ya nchi na kuingiza ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na malighafi zinazotumika viwandani, kusaidia wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa za kilimo, kusaidia kutoa mitaji ya uendeshaji wa viwanda, kutoa dhamana ya kibenki kwa ajili ya kusaidia miradi ya miundombinu, biashara.
“Tunaamini kupitia mchango wetu wa huduma za kifedha kwenye sekta ya viwanda na kilimo tutakuwa tumeiunga mkono Serikali kufikia lengo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kufikia mwaka 2025,” alisema
Itembe aliipongeza TANTRADE kwa kufungua Kliniki ya Biashara ambayo itawaleta pamoja wadau mbali mbali wa biashara kutoka sekta binafsi na umma watakao toa majibu kwa changamoto mbali mbali za kibiasaha na kuongeza kuwa benki ya Azania ni moja ya wadau ambao watakuwepo kwenye kliniki hiyo kwa ajili ya kutoa suluhisho na ushauri kuhusiana na mambo mbali mbali ya kibiashara
Maonyesha ya Sabasaba ya mwaka huu ni ya 42 na yanabeba kauli mbiu “Undelezaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda “
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)