Mwanachama mkongwe wa chama cha Mapinduzi CCM Sophia Simba amevuliwa uanachama wake mara baada ya kikao cha kamati ya maadili cha CCM kukaa na kubaini alikisaliti chama wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka 2015. Kwa kuvuliwa uanachama huko Sophia Simba anapoteza sifa na nafasi nyingine alizokuwa akizishika ndani ya chama na kupitia chama.
Huku Adam Kimbisa na Balozi Emmanuel Nchimbi wakipewa onyo kali ya maandishi.Balozi Nchimbi naye ametakiwa kuomba radhi wanachama.
Wengine waliofukuzwa uanachama ni
1. Ramadhan Madabida
2. Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa
3. Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na
4. Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)