Muswada binafsi wenye lengo la kutungwa kwa sheria ya kuwalinda albino umewasilishwa kwenye kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda.
Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania.
Katika muswada huo, Bhanji ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu.
Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino. Mheshimiwa Shyrose Bhanji
"Ninamshukuru Mungu kwa fursa hii, " anasema Bhanji huku akisema kwamba kwake yeye jana ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwani hatimaye aliweza kuwasilisha bungeni muswada huo binafsi ambao unaoitwa The EAC Protection Of People with Albinism Bill 2017.
Mwanamuziki mahiri nchini Chege Chigunda aliandika katika page yake ya Instagram ambapo alimpongeza mbunge huyo kwa namna anavyofikiri na kutetea walemavu aliandika:
“Hongera sana Mbunge wetu wa Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji @shyrosebhanji kwa kupigania haki za ndugu zetu wenye ualbino. Hakika umeacha alama kubwa ya uwakilishi wako Tanzania na Afrika Mashariki. Tunajivunia.”
Kipande cha nakala ya muswada huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)