Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya (Kulia), akiongozana na Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wakielekea kwenye Wodi za wagonjwa katika Hospitali ya Temeke kwaajili ya Kutoa Misaada mbalimbali wakati wakiadhimisha sikukuu ya wanawake duniani iliyofanyika tarehe 8 Machi 2014
Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, wakiwa wamebeba boksi lenye maji tayari kwa kuwagawia wagonjwa mbalimbali wakati walipotembelea hospitali ya Temeke wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani.
Jackline Jackson, ambae pia ni mmoja wa wafanyakazi wa PPF akimpatia mfuko wa Sukari mgonjwa aliyemtembelea katika Hospitali ya Temeke wakati wafanyakazi wanawake kutoka PPF walipotembelea hospitali hiyo na Kutoa Misaada mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Sikukuu ya Wanawake Duniani
Mfanyakazi wa PPF, akifurahia jambo pamoja na Bi Lucy Raphael (kulia) mara baada ya Kuwabeba watoto mapacha waliozaliwa na Bi Lucy Raphael (kulia) katika hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam jumamosi tarehe 8 Machi 2014. Bi Lucy Raphael ni miongoni mwa watu waliofaidika na zawadi mbalimbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF kwa hospitali hiyo.
Afisa Mahusiano Wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akimkabidhi Chupa ya maji mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Temeke wakati wafanyakazi wanawake wa PPF walipotembelea hospitali hiyo na kutoa misaada mbalimbali wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Wanawake Duniani mnamo Machi 8, 2014
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya (Kushoto), akimvisha karatasi maalum (Pampers), mtoto aliyelazwa kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014 wakati Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa PPF, walipotembelea hospitali hiyo Jumamosi ili kuwafariji na kuwapatia misada wagonjwa baada ya kushiriki sherehe za siku ya wanawake Duniani.
Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya
(Kushoto), akimkabidhi karatasi Maalumu (Pampers) Mama wa mtoto aliyelazwa
kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014 wakati Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa PPF, walipotembelea hospitali hiyo Jumamosi ili kuwafariji na kuwapatia misada wagonjwa baada ya kushiriki
sherehe za siku ya wanawake Duniani.
.jpg)
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa misaada kwa wagonjwa kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Kushoto), akiwa amempakata kichanga, saa chache baada ya kuzaliwa na kubahatika kukutana na wafanyakazi wanawake wa Mfuko huo waliotembelea hospitali ya Temeke kwa nia ya kuwafariji na kuwapatia misaada mbalimbali Juammosi Machi 8, 2014. Ziara hiyo ni baada ya kushiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga.
Mmoja wa wafanyakazi wanawake wa PPF, akimkabidhi pampasi mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Temeke ambapo wafanyakazi wa PPF walitembelea na Kuweza kutoa Misaada mbalimbali wakati wakiadhimisha sikukuu ya wanawake Duniani mnamo Machi 8, 2014
.jpg)
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam, Erica Sendegeye(Wapili kulia), akimpatia mama huyu mzazi, karatasi maalum za kujivunga watoto(Pampers), wakati wafanyakazi wanawake wa Mfuko huo, walipotembelea wagonjwa kwenye hospitali ya Temeke jana, ambako walitoa misaada mbalimbali ya vyakula na vifaa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani. Wakwanza kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi mbalimbali wakati Wafanyakazi wanawake wa PPF walipotembelea Hospitali ya Temeke na Kutoa Misaada kwa Wagonjwa yenye Thamani ya Shilingi Milioni Mbili za Kitanzania.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi mbalimbali wakati Wafanyakazi wanawake wa PPF walipotembelea Hospitali ya Temeke na Kutoa Misaada kwa Wagonjwa yenye Thamani ya Shilingi Milioni Mbili za Kitanzania.

.jpg)
.jpg)




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)