Banda la Kampuni ya Diamond Motors kama linavyoonekana katika Viwanja vya Mlimani City jana wakati wa Uzinduzi wa Magari Mapya aina Ya Fuso FJ kutoka Kampuni ya Diamond Motors ambao ni wauzaji wa Magari aina ya Mitsubishi na Fuso.
Meneja Mkuu Baada ya Mauzo wa Kampuni ya Diamond Motors Tanzania, Bw Valerian Martin akiongea na Waandishi wa habari jana wakati wa Uzinduzi wa Magari aina Ya Fuso yaliyofanyika katika Viwanja vya Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Diamond Motors Limited Tanzania, Bw Vikram Verma akiwasha gari mpya aina ya FUSO FJ wakati wa uzinduzi wa Gari Mpya aina ya Fuso kwenye Viwanja vya Mlimani City Hapo Jana.
Mkurugenzi Mkuu baada ya Mauzo, Bw Velarian Martin akimwelezea sifa za gari aina ya Fuso FJ, mmoja wa wakazi wa jiji waliopata nafasi ya kutembelea banda lao lililokuwa katika viwanja vya Mlimani City jana wakati wa uzinduzi wa Magari mapya aina ya Fuso.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakisikiliza kwa makini sifa za gari mpya aina ya Fuso FJ wakati wa uzinduzi wa gari hizo kwenye viwanja vya Mlimani city hapo Jana.
Mmoja wa Wakazi wa Jiji la Dar akilikagua gari mpya Aina ya Fuso FJ iliyopo wakati wa uzinduzi wa gari mpya aina ya Fuso FJ kutoka Diamond Motors jana kwenye viwanja vya Mlimani City.
Hii ni moja ya gari mpya kabisa aina ya FUSO FJ kutoka Kampuni ya Diamond Motors iliyokuwa kwenye uzinduzi wa gari mpya aina ya FUSO, jana kwenye viwanja vya Mlimani city.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)