Kutoka kushoto (mstari wa mbele) ni Waziri wa Utumishi Mh.Celina Kombani,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Rehema Nchimbi,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mh.Emmanuel Mwiliko na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu wakiserebuka katika maadhimisho ya siku ya Baba wa Taifa katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.Wengine vi viongozi waandamizi serikalini walioalikwa kwenye maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Kikundi cha Ngoma za Asili cha ‘Hiyari ya Moyo’ kikitoa burudani katika Maadhimisho ya Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Mh.Balozi Job Lusinde akielezea misingi ya Mwalimu kwenye Maadhimisho ya Siku ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakijumuika pamoja kuadhimisha Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakijumuika pamoja kuadhimisha Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Umma na wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakijumuika pamoja kuadhimisha Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Na
Happiness Shayo-Utumishi
Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere anasifika kwa kujenga misingi ya kizalendo ya umoja wa kitaifa,kufuta ubaguzi wa rangi,dini
na kabila,kuweka usawa ,uadilifu na utii wa sheria ambavyo ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya
taifa.
Hayo yalisemwa mapema leo na
Mh.Balozi Job Lusinde katika maadhimisho ya Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square
mjini Dodoma.
Balozi Lusinde aliyekuwa
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alisema kuwa ili kuhakikisha misingi ya
kizalendo inatekelezeka Mwalimu Nyerere alisisitiza falsafa ya ujamaa kwa
wananchi iliyohimiza wananchi kuhamia vijijini. “Mwalimu aliamini kuwa
wananchi wote wakihamia vijijini kutakuwa na maendeleo na ndio maana alitaka watumishi wahamie
vijijini”alisema Mh.Lusinde.
Mh.Lusinde alifafanua kuwa Mwalimu
Nyerere aliamini kuhamia vijijini kutapelekea mgawanyo wa rasilimali ardhi utakaopelekea
kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji. Aidha,Mh.Lusinde alisema
kutotekelezwa kwa falsafa ya ujamaa kumepelekea migogoro ya ardhi inayoonekana
sasa.
“Hatukutekeleza falsafa ya
ujamaa ndio maana dhambi ya migogoro ya wakulima na wafugaji inaendelea
kutumaliza”alisema Mh.Balozi Lusinde.
Naye Waziri wa Nchi,Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani alisema kuwa ili
kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere Serikali imetunga sheria ya kuwaenzi Waasisi wa
Taifa.
Alisema kuwa serikali imefanikiwa
kupata eneo la kujenga kituo cha Kuwaenzi Waasisi wa Taifa ili kuendelea kuenzi
mambo mazuri ya Waasisi hao. “Serikali imepata eneo la
kujenga Kituo cha Kuwaenzi Waasisi wa Taifa letu lililopo eneo la Kiromo
Bagamoyo”alisema Mh.Kombani.
Aidha,Mh.Kombani alifafanua
kuwa pamoja na mambo mengine kituo hicho kitakuwa kinafanya kazi ya
kuzikusanya,kuhifadhi kumbukumbu,mali,vitu vyenye umuhimu wa kihistoria vya
Waasisi kwa mujibu wa sheria.
Pia,Mh.Kombani alisema ili
kuendelea kuwaenzi Waasisi wa Taifa serikali imefanikiwa kuzitambua taasisi na
AZAKI zinazomiliki kumbukumbu,mali na vitu vyenye umuhimu kihistoria ili
kuhakikisha zinatunzwa vizuri kwa maslahi ya Taifa.
Maadhimisho ya Kumuenzi
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Dodoma yameandaliwa na
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kupitia Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na
wananchi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)