Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Prof. Mbarawa akifungua maonyesho ya Tanzania Homes Expo. Kushoto ni Imani Kajula Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Kulia ni Oscar Mgaya Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC. Wengine ni viongozi wa Camel Cement and CAM Gas.
Sehemu ya umati wa watu wakitembelea watoa huduma za sekta ya nyumba.
NHC ambao ni kati ya wadau wakubwa wa sekta ya nyumba nao wapo.
Umati wa watu waliofika kutembelea maonyesho ya Tanzania Homes Expo.
Maonyesho makubwa ya sekta ya nyumba yajulikanayo kama Tanzania Homes Expo yamefunguliwa rasmi leo na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Prof. Mbarawa. Akiongea baada ya kutembelea mabanda mbali mbali alisema ‘’ Inafurahisha kuona watoa huduma mbalimbali binafsi na wa serikali wako hapa kutoa taarifa na kuonyesha masuluhisho mbali mbali ya ujenzi. Napenda kuchagiza umuhimu wa kutumia Tehama katika kuboresha maisha ya wakazi’’.
Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group ambao ni waandaaji na wamiliki wa Tanzania Homes Expo alisema ‘’ Ukuaji wa idadi ya watu na upatikanaji wa makazi havina uwiano sawa, hii ni changamoto ambayo inaweza kutatuliwa kwa kuwawezesha wananchi kuwa na makazi hivyo maonyesho ya Tanzania Homes Expo yanawawezesha wananchi kukutana na kufahamu huduma au kupata ushauri wa sekta pana ya makazi’’.
Maonyesho ya Tanzania Homes yamedhaminiwa na CAM Gas, Camel Cement, African Life, CRDB na NHIF.Maonyesho hayo yameanza tarehe 14 na yataisha tarehe 15.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)