Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa la Moravian Tanzania mjini Sumbawanga akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda aliyemteua kufanya hivyo baada ya yeye kukabiliwa na majumu mengine ya kitaifa. Awali Waziri Mkuu aliafiki mualiko wa Kanisa hilo katika kuongoza harambee hiyo ambayo imefanikiwa kupata zaidi ya Tsh. Milioni 58 zikiwepo fedha taslim zaidi ya shilingi Milioni 47 na nyingine zikiwa ni ahadi. Zimekuwepo pia ahadi za mifuko 30 ya Cement na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya akitoa neno la awali kabla ya zoezi hilo la harambee kuanza ambapo aliwaomba waumini na wageni waliofika katika hafla hiyo kutoa kwa moyo katika kuchangia kazi hiyo ya Mungu. Kwa kuanzia alitoa ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa ambayo ni milioni tano (5) na yeye mwenyewe kuchangia milioni moja. Aliendeleza harambee hiyo kwa kuwachangisha kwanza viongozi wa Serikali alioambatana nao na kuendelea na taratibu zingine kwa mujibu wa ratiba.
Askofu Mkuu Conerad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa akitoa neno katika hafla hiyo ambayo aliwataka waumini wa kanisa hilo kuchapa kazi kwa nguvu na kuepukana na uvivu ambao alisema ni ugonjwa mkubwa kuliko hata gonjwa la ukimwi. Alikemea pia tabia ya watu wengi kuwahusisha watu waliofanikiwa kwa jitihada zao wenyewe na imani za “Freemason” au “Ufisadi”.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika harambee hiyo baada ya kupewa fursa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa mchango wake, aliahidi mchango wa laki tano na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani hapo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga William Shimwela ambaye pia ni mwanakamati wa ujenzi katika kanisa hilo, Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal na nyuma yake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Mwaruanda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiendelea na zoezi la uchangishaji.
Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Sumbawanga wakimfagilia kwa shangwe Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal aliyachangia Tsh. Milioni kumi zikiwepo za kwake binafsi Mil. 7 na nyingine Mil. 3 kuchangiwa na wabunge wenzake. Picha Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)