Mholanzi
maarufu: Van Persie (wapili kulia) akipongezwa na wenzake baada ya
kufunga katika mchezo dhidi ya Crystal Palace jumamosi
Akizungumza na mshindi wa kombe la ulaya wa zamani Paddy Crerand katika mahojiano maalumu ndani ya MUTV, Van Persie ameweka wazi kywa anataka kukaa zaidi Man United.
“Nimebakiza
miaka mitatu katika mkataba wangu na nataka kukaa zaidi” nyota huyo
mwenye umri wa miaka 30 alisema. “Najua na nawaona watu walionizunguka,
kufanya maamuzi ambayo watu wataangalia nyuma na kusema “Ni maamuzi
mazuri?”. Sihitaji kitu hicho.
“Nahitaji kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu kadri itakavyowezekana”
Kushinda
kombe na United msimu uliopita ndio kichocheo kikubwa kwa Van Persie
kupenda kukaa klabuni hapo kwani hajawahi kushinda na Arsenal tangu
atwae FA Cup mnamo mwaka 2005.
Mabingwa: Van Persie akishangilia ubingwa mwezi mei mwaka huu
Kazi inaendelea: Van Persie alijiunga na United msimu uliopita akitokea Arsenal
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MSHAMBULIAJI wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Mashetani Wekundu, Manchester United, Robin van Persie (RVP) anataka uongeza mkataba wake licha ya kubakiwa na miaka mitatu katika mkataba wake wa sasa.
Van
Persie alifurahia maisha ya Old Trafford msimu uliopita baada ya kutwaa
kiatu cha dhahabu kwa mara ya pili na kuwasaidia Man United kutwaa
ubingwa uliokuwa unatetewa na Manchester City.
Hali
ilionesha fainda ya Mholanzi huyo kuihama klabu yake ya Arsernal na
kujiunga na wapinzani wakubwa wa klabu hiyo yenye makazi yake kaskazini
mwa London, Manchester United.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)