Mratibu
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Hidaya Mohammed akiongea katika
mkutano wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo leo
(Ijumaa, Agosti 23, 2013). Wengine kulia ni Wajumbe wa Tume hiyo Bw.
Omar Sheha, Dkt. Salim Ahmed Salim na Alhaji Said El-Maamry.
Baadhi
ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
wakimsikiliza Mratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Hidaya
Mohammed (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa majadiliano mjini humo
leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013).
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mzee
Omary Yahaya Mhando akitoa maoni yake katika mkutano wa Baraza hilo leo
(Ijumaa, Agosti 23, 2013) mjini Bagamoyo. Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Jumanne
Chiboko akitoa maoni yake kuhusu rasimu ya katiba wakati wajumbe hao
waliojigawa katika makundi. Mkutano huo umefanyika leo (Ijumaa, Agosti
23, 2013) mjini Bagamoyo.
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Omar Sheha (kushoto) akiongea na
baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo (kulia) ambao wataongoza majadiliano ya makundi kabla ya kuanza
kwa majadiliano kuhusu rasimu ya katiba. Mkutano huo umefanyika mjini
Bagamoyo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013) mjini Bagamoyo. (PICHA NA TUME YA KATIBA)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)