KESI YA SHEHE PONDA; ULINZI MKALI MISIKITINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KESI YA SHEHE PONDA; ULINZI MKALI MISIKITINI

Na Shakoor Jongo
KATIKA kuhakikisha amani ya nchi haitetereki kutokana na vuguvugu la kesi inayomkabili Shehe Issa Ponda, ulinzi mkali umeonekana kuimarishwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar hasa misikitini..........
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»


Sheikh Ponda Issa Ponda
Misikiti ambayo polisi wamekuwa hawakauki ni pamoja na Mtambani-Kinondoni, Kichangani-Magomeni, Palestina-Sinza, Idrisa-Kariakoo, Kwa Mnyamani-Buguruni, Mtoro-Kariakoo na misikiti mingine yenye wafuasi wengi wa kiongozi huyo.
Ijumaa ambalo limekuwa likipitapita maeneo hayo lilibaini kuwepo kwa mapolisi ambao wamekuwa wakirandaranda wakiwa kwenye pikipiki na magari, lengo likiwa ni kuhakikisha wafuasi wa kiongozi huyo wanakuwa kwenye utulivu.

Aidha, imebainika kuwa, watu wa usalama wa taifa pamoja na polisi waliovalia kiraia nao wamekuwa wakitinga misikitini na kufanya ibada na waumini wengine lakini wakiwa na jukumu lingine la kuhakikisha ibada zinaendelea bila kuwepo kwa uvunjifu wa amani.
Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa waumini katika Msikiti wa Mtambani aliyejitambulisha kwa jina la Hamad Juma, mkazi wa Makumbusho jijini Dar alisema anashangazwa na uwepo wa polisi katika maeneo hayo kwani wao hawana malengo ya kufanya vurugu ila pale itakapobidi watafuata sheria kwa kukusanyika au kuandamana.


“Hii kesi ya Ponda imetikisa nchi na inaendelea kutikisa, tumekuwa tukiona polisi wakirandaranda wakiwa na ‘yunifomu’ na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
“Ninachoweza kusema ni kwamba sisi tutaandamana pale itakapobidi lakini nawashauri Waislam wenzangu tuwe na subira, tuache vurugu na kikubwa tumuombe Mungu awe nasi katika kipindi hiki kigumu ambacho kiongozi wetu anapitia.

“Tuwe watulivu, tuache sheria ichukue mkondo wake lakini tunaiomba serikali ijue Ponda ana watu wengi nyuma yake ambao hawatakubali kuona anatendewa kinyume na haki,” alisema muumini huyo.
Jumatatu iliyopita, Shehe Ponda alisomewa mashtaka matatu katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro na baadaye alirudishwa rumande katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar.Chanzo Global Publishers Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages