Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Sekretariate ya Baraza la Mawaziri ambako watumishi wake wawili wameteuliwa kuwa manaibu Makatibu wakuu, ambao ni Injinia Angelina Madete (kulia kwa Rais) na Mhe. Consolata Mgimba (kushoto kwa Rais) mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu hao na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Manaibu Katibu wakuu mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu hao Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa tarehe 23 Agosti, 2013, katika viwanja vya Ikulu, amewaapisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.
Ifuatayo ni Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa leo.
1. MAKATIBU WAKUU
Ndugu Sophia Elias Kaduma
Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Jumanne Abdallah Sagini
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Uledi Abbas Mussa
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara
Dr. Patrick James Makungu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu Alphayo Japani Kidata
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Ndugu Charles Amos Pallangyo
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Ndugu Sihaba Said Nkinga
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Anna Tayari Maembe
Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
2. NAIBU MAKATIBU WAKUU
Ndugu Dorothy Stanley Mwanyika
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Fedha za Nje na Madeni)
Ndugu Consolata Philipo Mgimba
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Eng. Angelina Elias Augustine Madete
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais
Dr. Deodatus Michael Mtasiwa
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - AFYA
Ndugu Monica Lyander Mwamunyange
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi
Ndugu Regina Lucian Kikuli
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Ndugu Kagyabukama Edwin Kiliba
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI)
Ndugu Zuberi Mhina Samataba
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - ELIMU
Dr. Yamungu Kayandabila
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Prof. Adolf Faustine Mkenda
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (SERA)
Ndugu Mwitango Rose Shelukindo
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dr. Selassie David Mayunga
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Elisante Ole Gabriel Laizer
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amantius Casmiri Msole
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)