SHEIKH PONDA ATOKA HOSPITALI YA MUHIMBILI, APELEKWA GEREZANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SHEIKH PONDA ATOKA HOSPITALI YA MUHIMBILI, APELEKWA GEREZANI


Katibu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (pichani kushoto) leo  ametoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha  mifupa (MOI) alikolazwa kwa tiba ya jeraha la kinachosemekana kuwa ni risasi na kusemekana amepelekwa katika gereza ambalo halijatajwa. 
Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Almasi amethibitisha hilo na kusema madaktari walimruhusu Sheikh Ponda bakutoka wodini baada ya hali yake kiafya kuimarika na kuonekana hana sababu ya kuendelea kubaki hapo. 
Kuhusu habari kuwa alipigwa risasi, Bw. Almasi amesema Muhimbili walimpokea Sheikh Ponda akiwa na kidonda ambacho kilihudumiwa sehemu ingine kabla ya kupelekwa hna kwamba hawakumkuta na risasi mwilini mwake. Badala yake, alisema, walikifungua upya kidonda hicho na kukihudumia upya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages