Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Said Ali Mbarouk, akimkaribisha
Balozi Mgodogo wa Oman Salleh Suleiman Al-Harith Ofisini kwake alipofika
kujitambulisha, huko Wizarani kwake kikwajuni Mjini Zanzibar
Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Said Ali Mbarouk akimpa maelezo
Balozi Mgodogo wa Oman Salleh Suleiman Al-Harith juu ya mausiano ya
kidugu ya Zanzibar na Oman (kulia ya waziri)
Picha
ya pamoja ya Waziri wa Habari Utamduni Utalii na Michezo Said Ali
Mbarouk (alievaa koti), Balozi mdogo wa Oman Salleh Suleiman Al Harith
na Naibu Waziri wa Habari, utamduni Utalii na Michezo Bihindi Hamad
Khamis.
Na Mwanamgeni Amour na Amina Abeid (ZJMMC)
Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk ameshauri
kuanzishwa Utalii wa uwenyeji kati ya watu wa Oman na Zanzibar ili
kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Waziri
Mbarouk ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na Balozi mdogo wa
Oman aliepo Zanzibar Salleh Suleiman Alharith huko Ofisini kwake Mnazi
Mmoja Mjini Zanzibar.
Amesema
Oman na Zanzibar zimekuwa na uhusino wa muda mrefu na wananchi wa nchi
mbili hizi wamekuwa wakishirikiana katika nyanja mbali mbali za
maendeleo na utamaduni hivyo kuanzishwa kwa utalii wa uwenyeji utaizidi
kuimarisha uhusiano huo. “
Uhusiano wa kihistoria kati ya nchi mbili hizi umewezesha wananchi wa
nchi hizi mbili kudumisha mila na silka zao kwa lugha zote mbili,
Kiarabu na Kiswahili, ”alisema Waziri Saidi Ali Mbarouk. Aidha
wazirihuyo amemshauri balozi mdogo wa Oman kuwahamasisha wawekezaji wa
nchi hiyo kuja kuwekeza Zanzibar na kumueleza kwamba kumeandaliwa
mazingira bora na vivutio vingi vya kuwekeza nchini.
Waziri
Mbarouk ameiomba Serikali ya Oman kulifanyia matengenezo jengo la
kihistoria la Beit el Ajab ambalo liliporomoka mapema mwaka huu ili
liweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Aidha
ameitaka nchi hiyo kusaidia vifaa vya kiwanda cha uchapaji cha Serikali
kinachojengwa katika eneo la Maruhubi na kujengewa kiwanja cha Michezo
katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Nae
Balozi mdogo wa Oman amemshukuru Waziri Said Ali Mbarouk na kumuahidi
kuwa watayawasilisha maombi yao katika Serikali ya Oman na ameeleza
matumaini yake kwamba yatapatiwa ufumbuzi katika muda mfupi ujao
kutokana na uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya nchi hizi
mbili. Amesema
Oman wanajisikia fahari kusaidia ndugu zao wa Zanzibar na kusema kwamba
imeweka milango wazi kwa wananchi wa pande hizi mbili kujenga
ushirikiano wa karibu zaidi na kusaidiana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)