Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana
keshokutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield)
kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa 2013/2014.
Mechi
hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini
itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo
mshindi atakabidhiwa ngao.
Iwapo
dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa
kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda
kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na
bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti
vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A
watalipa sh. 30,000.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)