Mourinho
bado anaendelea kuiwinda saini ya Rooney, lakini ofa yake ya pauni
milioni 40 ilitupiliwa mbali na kocha wa United, David Moyes alisema
nyota wake hauzwi.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA
wa Chelsea, Mreno, Jose Mourinho ameunga mkono kauli ya kocha Alan
Pardew ambaye ametaka dirisha la usajili liwe linafungwa kabla ya kuanza
msimu mpya.
Kocha
huyo wa paka Weusi, Newcastle, Pardew, amechukizwa na kitendo cha
Arsenal kuendelea kumshawishi kiungo wake Yohan Cabaye ili wamsajili,
hivyo ametaka dirisha liwe linafungwa kabla ya kuanza mechi za kwanza za
ligi kuu ili klabu pinzani kuacha kuwachanganya wachezaji wa timu
nyingine.
Na
sasa kauli hiyo iliyoungwa mkono na Mourinho itakuwa na maana Old
Trafford, kwani bosi huyo wa Chelsea anamuwinda mshambuliaji wa
Manchester United, Wayne Rooney – kabla ya kufungwa kwa dirisha la
usajili.
“Hakuna
kilichobadilika, kiukweli naungana na Pardew kuwa dirisha la usajili
linachelewa kufungwa, hadi mechi ya tatu na nne ndio linafungwa,
hapana”. Alisema Mourinho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)