Range Jackson akiambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maaalum(Matatizo
ya akili katika kujifunza jamii imezoea kuwa ita Tahila) walimu wa VETA wanakataa kuwaita jina hilo kwa
kuwainyesha kuwa wanafundishika ,Pichani akiwaonyesha askari Polisi waliotembelea katika banda lake
kifaa maalumu kinachotumika kumsaidia kumfunza.Kutokana na tatizo lake walimu
wa VETA wamelazaimika kumfundisha mtoto na baba yake mzazi Jackson Range ili
kumrahishia mafunzo yake kwa sababu baba atakuwa anakmkubushia masomo yake
aikiwa nyumbani kwa sababu mtoto huiga
mambo mazuri kutoka kwa wazazi .Katikati ni mwalimu wao Kintu Kilanga.Wananchi
mnakaribishwa katika banda la Mafunzo ya Ufundi stadi VETA, mjionee mafunzo
mbalimbali yanayotolewa na chuo hicho kwa vijana wetu.
KAZANA UTAELEWA TUU,Mwalimu waufundi
wa kuunga vyuma (Werding) Kintu Kilanga akimfuatilia
mwanafunzi wake Range Jackson wakati alipokuwa
akisaga chuma alichochomlea katika
monesho ya 37 ya biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, maarufu kwa jina la
Sabasaba.VETA wamekuwa wakitoa elimu juu ya mafunzo wanaoyotoa katika chuo
chao.
Mbunge wa viti maalum Magret Mkanga akipewa maelezo na Mwalimu wa ufundi
wa kuunga vyuma (Werding) Kintu Kilanga
juu ya elimu inayotolewa kwa Range Jackson (kulia) mwanafunzi mwenye mahitaji
maaalum(Matatizo ya akili katika kujifunza jamii imezoea kuwa ita Tahila)
wakati alipotembelea katika banda la VETA lililopo kwenye maonesho ya 37 ya
Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Mbunge wa viti maalum Magret Mkanga akikabidhiwa jiko na Range Jackson ambaye ni mwanafunzi
mwenye mahitaji maalumu wakati
alipotembelea katika banda la VETA, Katikati ni mwalimu wake Kintu Kilanga akishuhudia, Mafunzo ya Rangae
yanakwenda sambamba na baba yake hayupo pichani.
Mke wa Makamu wa Rais Asha Bilal na mke wa Waziri Mkuu
Tunu Pinda wakiangalia moja ya nguo
zinazotengenezwa na wanafunzi wa VETA wakati walipotembelea katika Banda hilo
jana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)