TANZANIA YAPENYA NUSU FAINALI PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANZANIA YAPENYA NUSU FAINALI PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

Mai mosi, Dar es Salaam; Jana usiku timu kutoka Kenya na Tanzania ziliwakilisha vizuzi  Afrika mashariki katika sehemu ya saba ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™. Timu ya Kenya ilifanikiwa kuzishinda timu nyingine na kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness. Kenneth kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi wamefuzu nusu fainali pamoja na watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao walipata nafasi ya pili jana usiku. 

Timu hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania sasa zina nafasi ya kuwakilisha Afrika mashariki na kushinda hadi dola za kimarekani 250,000 pamoja na kuvikwa taji la ushindi wa Pan-African, watakapoendelea hatua z juu zaidi. Timu hizi zitahitaji kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili kufanya vizuri katika hatua ya nusu fainali.

Timu zingine nne zitakutana katika robo fainali ijayo ili kuwania nafasi ya kuingia nusu fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.

Usikose kuangalia robo fainali za Pan-African kupitia televisheni za ITV na Clouds TV ambapo timu za Africa Mashariki zinapokutana na timu na timu zingine kutoka Afrika Magharibi huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali. -www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.


Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.



Notes to Editors:
The GUINNESS and FOOTBALL CHALLENGE, and GUINNESS VIP words and associated logos are trade marks

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages