Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu linatarajia kufanyika leo katika ukumbi wa BCIC mbezi beach kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 alfajiri lenye lengo la kuliombea Taifa Amani, Upendo na uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mlezi wa Aflewo (Africa Let’s
Worship) Askofu Fredy Kyara, alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza
kwa wingi kwani hakuna kiingilio.
Alisema kuwa, tamasha hilo litashirikisha kwaya mbalimbali kutoka makanisa 32 ya madhehebu tofauti katika kusifu na kuabudu.
Askofu kyara alisema, tamasha hilo linafanyika kwa mara ya tatu tangia kuanzishwa hapa nchini mwaka 2011 na kuenea nchi zote za Afrika.
“Tamasha hili limeboreshwa kwa kuongeza muiondombinu ya utendaji kazi, kwa kutanua wigo wa ushirikishwaji wa makanisa mengi,” alisema Kyara.
Aidha matasha mengine ya Aflewo, yanatarajia kufanyika nchi nzima kwa kufanyika kila mkoa, kwa mwaka huu litaanza kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Moshi na Zanzibar na hatimaye Afrika yote.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)