Na Hosea Joseph
USIKU wa Jumatano utabaki kuwa simulizi kwa mashabiki na wadau wa urembo katika jiji la Dar es Salaam ambao walifurika juzi usiku kwenye utambulisho wa warembo wanaowania taji la Redds Miss Kibaha 2013 uliofanyika kwenye ukumbi wa Club ya Kimataifa Club Bilicanas.
Warembo hao ambao walitambulishwa ikiwa ni sehemu Bilicanas pamoja na kuwajengea kujiamini wawapo jukwaani jambo ambalo walifanikiwa isavyo ikiwa ni pamoja na kulimudu jukwaa.
Warembo
hao ambao walipanda jukwaani saa saba na nusu usiku wakitambulishwa na
Kiongozi wa bendi ya The African Stars Entertainment Twanga Pepeta ambao ndiyo waliotoa burudani katika utambulisho huo.
Wakati wakipita jukwaani warembo hao walishangiliwa kuanzia
mshiriki wa kwanza hadi wa mwisho ambapo walikuwa washiriki 11 kati ya
12 ambao watapanda jukwaa Mei 17 katika ukumbi wa Conteainer Kibaha
.Kiingilio VIP ni sh. 10,000 na siti za kawaida shi 6,000.
Kalili
anawataja | wadhamini waliothibitisha kuling’arisha shindano hilo ambao
ni Michuzi Media Group (MMG), ASET, Chuo cha MC Donald Live Line
(Morogoro), Club Bilicanas, PR Promotion Company, Santorine Holiday
Resort (Kiluvya), Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake
cha Redd’s Premium Cold, Maji Umoja, Shear Illusions, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Multichoice Dstv, Image Pub, AKO Catering
Services Ltd, Panandi Panandi na Amazon Night Club.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)