
Majeruhi wa mlipuko wa bomu Arusha, Mwalimu Fatuma Tarimo akionyesha
kipande cha chuma baada ya kuondolewa kwenye mguu wake, katika
Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam jana. Picha na Michael Jamson
---
Bomu lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi
ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha,
inadaiwa lilitengenezwa kienyeji.
Wakati kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu
hao Regina Kurusei, (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9)
yanatazamiwa kufanyika leo Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
anatarajiwa kuhudhuria.
Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimdokeza
mwandishi wetu jana kuwa kwa ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu
hilo si la kiwandani akisema msingi wa imani yake ni jinsi vyuma
vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.
Watu saba wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.
Mstaafu huyo alieleza kuwa mabomu mengi zaidi ya
kienyeji hutengenezwa kwa kutumia bakuli za chuma, zikiwekewa baruti
ndani na kufungwa kwa waya.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)