GARI DOGO LAWAKA MOTO BAADA YA FUNDI KUCHOMELEA HUKU LIKIWA HALIJACHOMOLEWA BETRI MAENEO YA TABATA CHANG'OMBE LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

GARI DOGO LAWAKA MOTO BAADA YA FUNDI KUCHOMELEA HUKU LIKIWA HALIJACHOMOLEWA BETRI MAENEO YA TABATA CHANG'OMBE LEO

 Mmoja wa wakazi wa tabata chang'ombe akiangalia gari dogo aina ya corola iliyowaka moto mara baada ya fundi aliyekuwa anachomelea huku akiwa hajachomoa betri na kupelekea kuungua maeneo ya Tabata Chang'ombe
 Wakazi wa Tabata Chang'ombe wakiwa katika jitihada za kuzima gari hilo dogo ambalo limeungua kutokana na fundi kuchomelea huku akiwa hajatoa betri la gari hilo maeneo ya Tabata Chang'ombe Mapema asubuhi ya leo
Wakazi wa Tabata Chang'ombe Wakiangalia gari hilo dogo aina ya corola iliyoungua leo maeneo ya Tabata Chang'ombe mara baada ya fundi kuchomelea gari hilo huku akiwa hajachomoa betri na kupelekea kuungua. Picha Zote na Fransisca wa Lukaza Blog

Gari ndogo aina ya Toyota Corola imeungua kwa moto mapema leo maeneo ya Tabata Chang'ombe mara baada ya Fundi aliyekuwa anachomelea kuchomelea gari hilo huku akiwa hajatoa betri la gari hilo na kupelekea kuwaka moto ambao wakazi na majirani hao walijitahidi kuuzima kwa maji na mchanga lakini bila mafanikio na kupelekea gari hilo kugeuka ghafla chuma chakavu.

Gari hilo lilipelekwa na dereva ambaye aliliacha Kwa fundi huyo katika garage bubu maeneo ya Tabata Chang'ombe na yeye Kuelekea Kinyerezi kuangalia Shamba lake. Mara baada ya Kuliacha kwa fundi gari hilo lilianza kufanyiwa matengenezo na kupelekea Fundi huyo kuchomelea bila kutoa betri na kupelekea kuwaka moto ambao pamoja na jitihada za wakazi na majirani wa garage bubu hiyo kujitahidi kuuzima kwa mchanga na maji lakini walifua dafu.

Baada ya Kuonekana anayesemekana kuwa ni mmiliki wa garage bubu hiyo kuonekana akilia kwa uchungu sana na kupelekea watu kuhisi kuwa anawaza jinsi ya kulipa gari hilo na ndipo wadau wakabidi kumuuliza dereva huyo kuhusu gari hilo kama lina bima. Kwa Mujibu wa Dereva wa gari hilo ambaye ni dereva taksi ameuambia mtandao wa Lukaza Blog kuwa Gari hiyo ilikua haina bima kwa muda mrefu na kwahiyo kuungua kwa gari hii kumemfanya kuwa maskini na kupelekea kumpa mawazo sana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages