Ndoa
hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na
Wedding Ceremony Imaginations,bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi,na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali,Boonge la Shela kutoka Uturuki,Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni,Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall..
Je,umewahi kuwaza Mmeo
au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia??Umewahi kuwaza
Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani??Mtakapokosa
watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba
unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi??Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya
Harusi.Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu
mazito na Kiapo kisichovunjika.Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali
kidoogo...
Je,Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex
watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex
wako???Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya
kuanzia maisha??Sidhani...Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani
Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????Alamsiki...!OMBA MUNGU AKUEPUSHE NA MABAYA YOTE KATIKA NDOA KWANI NDIO KIMBILIO LETU..(Kweli Cheka Upate Afya)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)