Zifuatazo ni baadhi ya taswira za Rama mla watu enzi hizo:
Rama
na mama yake, Khadija Ally wakipelekwa mahakamani chini ya ulinzi mkali
baada ya kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Salome yaliyotokea
Aprili 25, mwaka 2008.
KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija
Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya
kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu)
alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla
Watu, ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga
mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa
huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Khadija Ally yeye
ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya
kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome. (PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)