Afisa Masoko wa PSPF Bi. Hawa Kikeke akitoa maelezo kuhusu Mfuko wa
Pensheni wa PSPF kwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Gharib
Bilal kwenye maonyesho ya 8 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Diamond Jubelee Dar es
Salaam. Alifafanua kwamba sasahivi sheria inaruhusu wafanyakazi kujichagulia
wenyewe Mfuko wanaopenda kujiunga nao bila kuchaguliwa na Mwajiri pindi tu
wanapopata hajira mpya.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Ndugu Ntimi Mwakajila
akiwaelezea wanafunzi wa vyuo vikuu juu ya fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko
ikiwemo mpango wa kuchangia kwa hiari.
Mhandisi Ujenzi mwandamizi Ally Shanjirwa akielezea kuhusu nyumba
zilizojengwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya kukopesha wanachama
wake. Nyumba hizo zimekwisha jengwa
katika mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Morogoro, Mtwara na Tabora. Lakini mchakato wa ujenzi huo unaendelea
katika kila mkoa Tanzania. Nyumba hizo
zinakopeshwa kwa wanachama kwa marejesho ya kila mwezi kwa muda wa miaka
25. Mteja huyo alitembelea banda la
PSPF kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya
Usajili wa Wakandalasi Mlimani City Dar es Salaam
Afisa Mwandamizi Uendeshaji Bi. Sophia Mbilikira akielezea aina
mbalimbali za Mafao yatolewayo na Mfuko wa PSPF pamoja na mikopo ya
nyumba. Afisa huyo alisema sasahivi
sheria inaruhusu mtu kuendeleza michango yake hata kama akiacha kazi kutoka kwa
mwajiri wake alipoanzia kazi na kwenda kwa mwajiri mwengine bila kupoteza
uanachama wake. Aliyasema hayo kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa
Wakandarasi Mlimani City Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi Masoko wa PSPF Bi. Queen Edward akitoa mada kwa
wadau wa Makandarasi Tanzania kwenye
Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi unaofanyika Mlimani City Dar es Salaam. Afisa huyo alisema Mfuko wa PSPF unachukua
mtu yeyote kutoka kwa mwajiri yeyote hata kama siyo wa serikalini, na kwa wale
ambao wameshakuwa wanachama wa Mifuko mingine ya Hifadhi ya Jamii wanaweza
kujiunga na PSPF katika mfumo wa uchangiaji wa hiari.
Afisa mwandamizi Masoko wa PSPF Bi Edward Queen
akijibu hoja mbali mbali zilizotolewa na wateja waliotembelea banda la Mfuko
huo lilikuwepo Mlimani City conference centre wakati wa Mkutano wa Mwaka wa
Bodi ya lUsajili wa Wakandarasi Tanzania
unaofanyika Mlimani City Dar es Salaam
Makandarasi wa Tanzania wavutiwa na nyumba za PSPF pamoja na huduma
zilizopo katika Mfuko huo. Afisa Mwandamizi
wa PSPF Bi. Sophia Mbilikira akitoa maelezo kwa wakandarasi waliokuwa
wakitembelea banda la PSPF katika
Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Mlimani City Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)