Dar
es Salaam kupitia televisheni za ITV na Clouds TV jana usiku katika
kipindi cha 8 cha Guinness Football Challenge (robo fainali ya 3) Ghana
waliweza kuibuka vinara na kupata dau kubwa zaidi tangu mashindano
haya yaanze na kufuzu kuingia nusu fainali. Jonathan Naab na Desmond
Odaano kutoka Afika Magharibi waliweza kuhimili vishindo na vikwazo
vyote hata kufikia hatua ya mwisho ya Ukuta wa pesa wa Guinness ambapo
walijishindia taslim dola za kimarekani 3,000 na kufanya kuwa na jumla
ya dola 8,500 kutokana na dola 5,500 walizokua nazo awali.
Wawakilishi
kutoka Ghana wataiwakilisha nchi yao katika nusu fainali pamoja na
wawakilshi kutoka Kenya ambao nao wamefuzu kuingia nusu fainali Ephantus
Nyambura na Samuel Papa, ambao pia walifanya vizuri ingawa hawakufikia
hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Timu
nne mpya zitaingia uwanjani katika robo fainali ya mwisho wiki ijayo
nakuona kama wawakilishi wa mwisho kutoka Afrika Mashariki watatutoa
kimasomaso na kufuzu kuingia nusu fainali
Robo
fainali ya tatu ya Pan-African itarushwa kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana
vikali na nchi zingine za Afrika. Usisahau kuwa na chupa ya bia
uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki
Hakikisha unaufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na
kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia
kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV
kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)