HATIMAYE SHEKHE PONDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA NJE HUKU WENZAKE WOTE 49 WAKIACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HATIMAYE SHEKHE PONDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA NJE HUKU WENZAKE WOTE 49 WAKIACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU

Akiwa na furaha baada ya hukumu yake kumalizika leo katika mahakama ya kisutu jijini dar es salaam
Akitetra jambo na baadhi ya watu!
Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.
Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhuluma tunayofanyiwa waislamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.
Tutatoa tamko!
Kuna mengi yamejitokeza na wale waliokuwa wakiogopa sasa wamepata somo!
Safari ikaanza!
Akapewa ulinzi tena!
Akaingia kwenye gari!
Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa gari lake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito kwenye mataa ya Maktaba Square. 
Wafuasi wakajimwaga barabarani!
Takbirrrrrrrrrr!Allahu Akibarrrr! ndio maneno yaliyokuwa yakitamkwa hapo
Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wa gari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.
Waliufukuza msafara huo hadi pale ulipotokomea!
Kaaaazi kwelikweli!
Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kuwakimbia.
Waumini wa Kiislamu wakiwa Wammbeba Juu mmoja wa aliyekuwa mshtakiwa mwenza na Shekhe Ponda Mara baada ya Kuachiwa Huru leo Katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu.
HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili na kuonekana hawana kesi ya kujibu. Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha Mwaka Mmoja nje kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.

Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo paliibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waislamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.

5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waislamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.
Tumewashinda!
Furaha!
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!
Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.
Barabara nazo zikavamiwa na wafuasi hao.
Hoyoooooooooo!
Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.
Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia!
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari yoyote ambayo ingeweza kujitokeza
Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa maeneo ya mahakamani hapo
Kama kawaida walikuwepo pia!Picha Kwa Hisani ya Audifance Jackson

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages