EURO-MASTERCARD VISA-EMV COMPLIANT KUANZA KUTUMIKA KWENYE MABENKI YOTE NCHINI TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

EURO-MASTERCARD VISA-EMV COMPLIANT KUANZA KUTUMIKA KWENYE MABENKI YOTE NCHINI TANZANIA

2-NW wa Fedha Mkuya
Naibu Waziri wa  Fedha, Saada Mkuya NMB
 Immaculate Makilika- Maelezo.

SERIKALI  imesema kwamba Benki ya NMB inatarajia kuanzisha utaratibu wa kutuma ujumbe wa simu  kwa wateja  kupitia simu zao (Bank massage) pindi mteja atakapofanya muamala  ili yule mwenye akaunti aweze kukubali  au kukataa au kufahamu kuwa kipindi  hicho akaunti yake  inatoa au inatumika kutoa fedha.

Aidha, Serikali imefafanua kuwa  imezitaka benki zote kutumia  teknolojia  ya kisasa ya (Euro Mastercard Visa-EMV Compliant) ambayo hutumia mfumo wa “chip based” na kuachana  na mfumo wa kizamani  unaotumia “magnetic stripe”. Ambao kwa sasa umepitwa na wakati na ni rahisi kwa wahalifu kuuchezea na kuiba  fedha za wateja.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma wakati Naibu Waziri wa  Fedha, Saada Mkuya  alipokuwa akijibu swali la Kidawa Hamid Saleh(Viti Maalum – CCM) alipouliza je,Serikali  ina mkakati gani wa kupambana na matatizo ya wizi wa Mabenki kwa njia ya mtandao.

Alisema   kupitia Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali katika juhudi za kupambana na  tatizo la wizi kwa njia ya mtandao.

Aidha Naibu waziri alisema hatua zingine za kukabiliana na tatizo hili la mabenki ni kuweka mfumo  wa “Anti- Skimming  Devices ambapo mfumo  huu unazuia mwizi kugundua  namba ya siri ya mteja(PIN), na kwa upande wa Benki ya NMB imeamua kusimamisha utaratibu wa “swapping” uliokuwa unatekelezwa na kampuni ya simu ya Airtel.

Katika swali la nyongeza Kidawa aliuliza pia kama Serikali imewapa  adhabu yeyote wafanyakazi wa NMB na Airtel waliobainika kuhusika na upotevu wa fedha za wateja na je kama  Benki ya NMB  itarejesha fedha hizo kwa wateja?

Mkuya alijibu maswali hayo kwa kusema kuwa bado hajajua namna gani NMB na Airtel imewaadhibu wafanyakazi wake, isipokuwa kuhusu kurejesha fedha kwa wateja  ndio NMB  inafanya hivyo.

Aidha Naibu waziri huyo aliendelea kwa  kusema  Serikali inakamilisha sheria ya wizi kwa njia ya mtandao (Cyber Crime Act) ambayo itasaidia  kupunguza tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages