Washindi
wa kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge Ken Muturi
(kushuto) na Chris Mwamgi(kulia) wakishangilia ushindi walioupata huku
wakiwa wamebeba pesa taslimu walizojishindia katika shindano hilo jana
usiku na pembeni ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Lary
Asengo(anayepiga makofi kulia).
………………………………………………..
Jana
usiku kupitia Televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Tanzania
ilishindwa kutumia nafasi ya kipindi cha mwisho cha mashindano ya “Guinness
Football Challenge” katika hatua ya Afrika Mashariki baada ya kutolewa
na timu kutoka Kenya. Rangi nyekundu imeonekana kuwa ni rangi ya bahati
kwa timu za Kenya kwani hii ni timu ya nne kutoka Kenya kufanikiwa
kufuzu kuingia hatua ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGETM.
Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ndio walioibuka washindi jana usiku
kwani walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta wa
pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola za kimarekani 1,500.
Ni
vipi Kenneth na Chris wataweza kumudu hatua ya Pan-African? Sasa wana
nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano ya Pan-African ambapo
watakutana na wawakilishi pekee kutoka Tanzania, Daniel Msekwa na
Mwalimu, washiriki kutoka Uganda Alex Muyobo na Ibrahim Kawoova pamoja
na wenzao kutoka Kenya,Francis Ngigi na Kepha Kimani(washindi wa kipindi
cha 2), Kenneth Kamau na Wills Ogutu(washindi kipindi cha 3) na
Ephantus Nyambura na Samuel Papa(washindi kipindi cha 4).
Timu
hizi tano zitakua uwanjani kutimiza malengo yao, ambapo watakutana uso
kwa uso na washiriki kutoka Ghana na Cameroun kuonesha ni nani ana
maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu, hata kuvishwa ubingwa wa
Pan-African na kuondoka na dola za kimarekani 250,000.
Usikose kuangalia mashindano haya kupitia televisheni za ITV na Clouds TV huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.
Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)