Mlipuko umetokea katika kiwanda
cha kutengeza mbolea karibu na Waco, katika jimbo la Texas nchini
Marekani huku idadi kubwa ya watu wakijeruhiwa na wengine kukwama ndani
ya kiwanda hicho
Moshi mkubwa uliokena ukipanda
juu kutoka katika eneo la mlipuko. Wazima moto na magari ya Ambulance
pamoja na helikopta sita zilionekana zikiwasaidia majeruhi.
Wazaima moto hapa wakipambana na
moto huo karibu na kiwanda hicho. Majengo kadhaa yaliharibiwa vibaya
mengina yakiwa katika maeneo jirani.
Wazee waliokuwa katika makao
jirani ya kuwatunza wazee, walihamishwa mara moja. Kulikuwa na ripoti
kuwa wazima moto walikuwa wanajaribu kuzima moto wakati mlipuko huo
ulipotokea.
Uharibifu mkubwa ulitokea kwa
makao ya kuwahifadhi wazee. Mlipuko ulitokea nyakati za usiku wa kuamkia
leo
Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa katika mulipuko
uliotokea kwenye kiwanda cha mbolea kilichoko Kaskazini Magharibi mwa
eneo la Waco, jimbo la Texas. Wengi wamekwama ndani ya majengo
yanayendelea kuteketea kufuatia mulipuko huo.
Meya wa Mji kulitokea mulipuko huo, Tummy Muska
ameelezea kutokea moto mkubwa uliolipuka sawa na bomu. Mulipuko huo
umeharibu majengo ya kiwanda hicho, makaazi ya karibu kikiwemo kituo
kimoja cha afya.
Wazima moto, magari ya kubebea wagonjwa na helikopta sita zimetolewa kushughulikia majeruhi na kutuliza hali ya sasa.
Majengo kadhaa yameendelea kuteketea karibu na
kiwanda hicho cha mbolea.Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema
zinasea kuna watu waliopoteza maisha.
Dean Wilson wa idara ya usalama ya Texas amesema nyumba 75 karibu na jengo hilo ziliharibiwa kabisa.
Amesema kufikia sasa hawezi kuthibitisha vifo
vyovyote. Watu 38 wameripotiwa kua katika hali mahututi. Makundi ya
wokozi yameanza kufika nyumba hadi nyingine kuwaokoa majeruhi na kutoa
huduma ya kwanza.
Kituo cha Dharura kimewekwa kwenye uwanja wa
mpira ulioko karibu.Gavana wa Texas amesema afisi yake imetoa raslimali
zake kusaidia katika juhudi za wokozi.
Chanzo: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)