Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema, leo amepandishwa kizimbani
jijini Arusha na kusomewa shitaka lililokuwa likimkabili na kuachiwa kwa
dhamana iliyokuwa na masharti rahisi.
Godless
Lema, alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani humo kwa tuhuma za
uchochezi wa vurugu zilizosababishwa na wanafunzi kwenye chuo cha
Uhasibu mwanzoni mwa wiki iliyopita mwenzao kuuwawa huko maeneo ya njiro
jijini humo.
Mbunge huyo alikamatwa siku ya Ijumaa na kuwekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Baada
ya kuachiwa mahakamani hapo mbunge huyo ameongozana na wafuasi wake kwa
msafara wa maandamano na mapikipiki kuelekea katika Ofisi za Chama
hicho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)