Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akiongea na Mshindi wa Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin Michael.
Kutoka kushoto,Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu,pamoja na Meneja wa Huduma za ziada wa kampuni hiyo, Bw. Benjamin Michael,wakichezesha droo ya mwisho ya "MAHELA"ambapo Bw.Valelian Nickodemus(22)Mwanafunzi wa Chuo cha uwalimu Mkoani Kigoma alijishindia kitita cha shilingi Milioni 100,kupitia promosheni hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumpata mshindi wa Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Mlau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin Michael.
Hatimaye Mshindi wa Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela amepatikana ikishuhudia Mwanafunzi chuo cha Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian Nickodemus(22) akiibuka mshindi kupitia droo kubwa iliyochezeshwa leo jumatatu.
Mshindi huyo amepatikana miongoni mwa mamilioni ya washiriki walioshiriki kucheza katika promosheni hiyo, Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu Mshindi huyo ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kumuwezesha kushinda kiasi hiko kwani hayakuwa mategemeo yake katika maisha yake.
"Watu wengi hawakuwa wanaamini kuwa Promosheni hizi ni za kweli, Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa moja katika Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na mzee niliamua kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, Hakika nimefurahi sana na ninawashukuru Vodacom, alisema Nickodemus.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amewapongeza Wateja wa mtandao huo kwa kushiriki katika promosheni hiyo na kumpongeza kwa upekee mshindi wa Promosheni hiyo na kujinasibu kuwa anajivunia mafanikio ambayo Promosheni hiyo imeyapata kwa kufanikiwa kubadili maisha ya mamia ya Watanzania.
"Sisi kama Vodacom tumefurahi kwa kumpata mshindi wetu wa mwisho ambaye ameibuka kidedea kati ya Mamilioni ya Watanzania lazima tukiri kuwa ni bahati kubwa na tunatoa pongezi za kipekee kwa mshindi wetu, alisema Twissa na kuongeza kuwa "Zaidi ya yote tunajivunia kwa upekee kabisa namna ambavyo promosheni hii imebadilisha mamia ya maisha ya Watanzania, Tumepata washindi kutoka katika Nyanja mbalimbali wakiwemo wakulima, wafanya biashara ndogondogo wanafunzi pamoja na wastaafu wengi ambao nao wameendelea kuboresha maisha yao.
Tangu Promosheni ya MAHELA kuzinduliwa tarehe 24 Mwezi wa kwanza na washindi 333 wamepatikana na kushuhudia kiasi cha Shilingi milioni 480 zikitolewa hadi sasa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)