WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo Jumamosi, Machi 2, 2013 atakutana na Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa Februari 18, mwaka huu.
Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
Tume hiyo inajumuisha wadau
kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association
of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO),
Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
Wadau wengine wanatoka Chama cha
Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Katika matokeo hayo
yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya
mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)