Milioni 5 kwa mwezi zinavyoangamiza michezo ilala - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Milioni 5 kwa mwezi zinavyoangamiza michezo ilala

Tabu shaibu ambaye ni msemaji wa Manispaa ya Ilala akielezea namna walivyoutwaa uwanja huo.Picha na Tanpress
 magari yakiwa yameegeshwa kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuuzwa na kuoshwa,picha na Tanpress
 Mlinzi Akiwa Kazini
Shule ya Sekondari ya Dar Es Salaam

Na Mwandishi wetu,Tanpress
 
*amri ya rais kikwete yapuuzwa
*Wadau watishia kufanya maandamano kuokoa uwanja wa kidongo chekundu
*Meya adai anayetakaa mazoezi achezee nyumbani kwake.

 
Mchungaji Mtikila alifikia hatua hiyo baada ya manispaa ya Ilala kumuuzia mwekezaji viwanja vya amnazi mmoja ajenge hoteli lakini kwa bahati nzuri Mtikila aliibuka kama nabii akaukoa sasa hivi wamerudi tena.   
 
Je wewe ni mdau wa michezo hususani Soka? Unakumbuka kuwa muda mfupi tu baada ya Rais  Jakaya Kikwete kuanza kazi katika Ikulu ya Magogoni alitangaza kurejeshwa viwanja vyote vya wazi vilivyokuwa vimeporwa na wajanja wakavigeuza matumizi?
 
Hakuna takwimu kamili ni viwanja vingapi vilivyorejeshwa lakini kinachokumbukwa ni ile amri ya Rais aliyosema wazi kuwa viwanja vya wazi viachwe ili kila anayetaka kucheza acheze…
 
Rais Jakaya Kikwete akiwa pia  mdau mhimu wa michezo alijua umhimu wa kuawaacha viwanja hivyo kwa matumizi ya michezo na kizazi kijacho ,lakini leo miaka mitano baada ya agizo hilo Manspaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, wamevunja amri hiyo.
 
Kifupi ni kwamba wametwaa kwa makusudi uwanja mhimu wa kidongo chekundu uliokuwa unategemewa na wadau wa michezo na kuufanya kitegauchumi cha watu wachache.
 
Hivi sasa wamegeuza matumizi ya uwanja huo kutoka uwanja wa mpira na michezo mingine kuwa soko la magari ya mitumba,gereji bubu na eneo la kujifunzia magari kwa wanafunzi wanaotaka kuwa madereva.
 
Kitendo hicho kiliwaudhi wadau wa michezo wilaya hiyo ambao walifikia hatua ya kutaka kuandamana ili wautwae kwa nguvu uwanja huo ambao upo kwenye historia ya viwanja vikongwe nchini.
 
Baada ya taarifa hizo kusambaa jukwaa la habari kupitia shirika lake la habari nchini (TanPress) liliamua kufanya uchunguzi kubaini kilichojili nyuma ya kashfa hiyo ambayo inaweza kuleta picha mbaya kuwa watendaji wa Manspaa ya Ilala wamempuuza Rais wananchi.
 
 Kwanza Manispaa ya Ilala inaongozwa na Mnec-CCM ,Meya kijana  JERRY SILAA ambaye akizungumzia kadhia hiyo baada ya kuhojiwa na Tanpress alisema kuwa “kwanza ni kuambie ule  uwanja tuna maelekezo maalumu kutoka kwa rais Kikwete”amenukuliwa na Tanpress.
 
Meya Silaa alipoulizwa kama anakaumbuka amri ya rais kuwataka viongozi kueheshimu viwanja vya wazi na kwuaachia watoto wacheze, kwa yeyote anayetaka hivyo kama wameamua kugeuza eneo hilo kuwa maegesho na soko la magari mabovu alihamaki.
 
“Sikiliza wewe mwandishi ustake kutuchonganisha na Rais..ambaye ni mwenyekiti wangu. Nimesema kuwa tumezungumza naye kabla ya kubadilisha huo uwanja lakini lazima mjue kuwa sisi ndio mafather City hivyo masuala ya michezo achana nayo sisi tunatazama miaka 25 ijayo”Meya Silaa amesema.
 
Diwani huyo wa kata ya Gongo la Mboto Jimbo la Ukonga ambaye ni kijana mdogo anayepaswa kulinda na kuetetea viwanja vya michezo amesema kuwa eneo linalolalamikiwa ni mali ya Manispaa hivyo wanaweza kulibadili kwa matumizi yoyote wanayoona yanafaaa.
 
Meya ameuliwa kwamba haoni kuwa akiwa mjumbe wa NEC-CCM amekwenda kinyume na maagazo ya mwenyekiti wake wa CCM aliyesema viwanja vya michezo visijengwe? 
 
“Aha ha be care fuly nani kwakwambia tumekiuka utaratibu wa mwenyekiti ...kwanza huwa sifanyi mahojiano na mwandishi bila kurekodiwa ..nimekuheshimu sana sasa ntakustaki ukinichonganisha na mheshimiwa.......

“...........Kwanza nani kwakumbia kuwa lile ni eneo la michezo? Sisi kama wamiliki wake tunajuwa kuwa ni eneo la wazi ambalo lilikuwa linasubiri kupangiwa shughuli yoyote, sasa tumeona wakati huo bora tugeuze liwe eneo la kutunzia magari kwa muda wakati huo tunatafuta mwekezaji ajenge maegesho”anasema 
 
Hata hivyo baada ya kuulizwa ni wapi wanamichezo wa ilala watakapokuwa wanatumia kucheza alisema kwa haraka “ wamabie waende Jangwani...ndipo kuna kiwancha cha michezo wanapaswa (kuturoti) kukimbia hadi jangwani wakifika kule wanakuta miili inachemka”

Mstahiki Meya anasema kuwa katika suala la michezo halina kipaumbele sana katika Manispaa yake kwani sio suala la maendeleo ‘hatuwezi kuacha kukusanya mapato katika uwanja ule pesa ambayo ingetumika kutengeneza madawati au kujenga shule tuwachie watu wanacheza ..kachezeni Jangwani ukijaa kila mtu afanyie mazoezi nyumbani kwake............”
 
Baada ya majibu hayo yenye kukatisha tamaa kwa wadau wa michezo TanPress iliamua kuzungumza na baadhi ya wadau wa michezo waliokuwa wanautegemea uwanja huo  kwa shughuli za michezo ambao ni shule ya Sekondari Dar es SALAAM,Gerezani na Shule ya msingi Gerezani.
 
Walimu hao wenye dhamana na michezo shuleni kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakihoji uhalali wa Manispaa ya Ilala kugeuza eneo hilo matumizi bila kuwashirikisha kwanza huku ikitambua kuwa shule hizo hazina eneo lingine la michezo.
 
“Sawa hata kama wakidai kuwa eneo hilo ni la Manispaa hata sisi shule hizi ni mali ya Manispaa kwa hiyo tuna haki ya kulalamika ...kwanza hiki ni kipindi cha michezo (UMISETA) huo uwanja tunauhitaji sana lakini hatuna namna”anasema Mwalimu wa Shule ya Dar es Salaam.
Walimu wa Sekondari hiyo wanasema kuwa shule yao ambayo inamuunganiko wa shule nyingine ya Gerezani hawakutegemea serikali kupora uwanja wa shule bila kuwashirikisha na kuwasikia mawazo yao.
 
Kwa upande mwingine walimu wa shule ya msingi Gerezani wao kwanza waliogopa kuzungumza na shirika hili ambalo linafanya kazi ya kukusanya matukio na kusambaza kwenye vyombo vya habari baada ya kuelimishwa walianza kutoa maoni yao.
 
Mwalimu kuu wa shule hiyo na Mwalimu wa michezo walisema walianza kwa kusema kuwa shule yao haina uwanja wa michezo na walikuwa wakitegemea kiwanja hicho eneo mhimu lakini wameshangaa kukuta kimegeuzwa kuwa mnada wa magari.
 
Walimu hao walisema kuwa baada ya kuuliza kwenye uongozi wa manispaa hiyo waliambiwa kuwa  wakitaka kucheza ,wakacheze kwani uwanja huo ni mkubwa lakini walipojaribu kuutumia ikashindikana kutokana na kwamba kuna watu wanautumia kujifunzia magari hivyo wanaweza kugonga watoto.

Wakati hali ikiwa hivyo taarifa kutoka ofisi ya mahusiano Ilala, zinasema kuwa Mkandarasi aliyetajwa kwa jina la Butiama Provision Store ndio ilipewa mkataba wa Miezi sita kukusanya ushuru eneo hilo kwa makubaliano ya kukabidhi shilingi Milioni 5,700,000 kwa mwezi.
 
Hata hivyo Tanpress iliwasiliana na msemaji wa Manspaa hiyo Tabu Shaibu ili kupata ufafanuzi zaidi wa sakata hilo ambapo alisema kuwa ni kweli eneo hilo wameamua kujenga ukuta na kuruhusu magari yaliyokuwa yanasimama barabara ya Lumumba yaingia ndani ili Manispaa iweze kujipatia kipato.

Tabu alisema kuwa anashangaa kuona hivi sasa watu wanaibuka na kulalamaikia uwanja huo wakati ulijadiliwa kwenye kamati za mipango miji na kama kulikuwa na tatizo maafisa michezo wa manispaa ya Ilala kwa niaba ya wadau wa michezo wangeweza kutoa ushauri kabla hilo halijafikiwa.
 
“Hili suala mbona lilijadiliwa kwenye vikao hadi likapitishwa barazani anayelalamika sasa ni nani mara tunasikia kuna watu wanapanga kuwandamana ........tumegeuza eneo hilo sehemu ya magari kwa muda wakati huo tukimtafuta mwekezaji ambaye atakuja kuekeza katika shughuli zinazofanana na zile za awali ambazo ni michezo”amaenukuliwa Shaibu.

Viongozi wa serikali kubadilisha viwanja kinyume na utaratibu  bila kuwauliza wananchi tabia hiyo haikuwanza leo kwani hata katika jiji la Mwanza kama sio wadau kusimama imara tayari Halmashauri ya jiji hilo ilikuwa imeazimia kubadilisha uwanja mkongwe wa Nyamagana kuwa eneo la ujenzi wa hoteli binafsi.
 
Hali hiyo ilipigiwa kelele kwa nguvu hadi viongozi wa Wizara ya ardhi wakaingilia kati na kuun sulu uwanja huo kwa madai kuwa ni eneo la wazi ambalo linaweza kutumika kuwafadhi wananchi eneo litataoakea tetemekokubwa au kuzuka moto.
 
Jijini Dar es Salaam, pia wananchi wake bado wanakumbukumbu na Manispaa hiyo ya Ilala iliwahi kutaka kumuuzia mwekezaji uwanja wa Mnazi mmoja ajenge hoteli yake kubwa lakini kwa bahati eneo hilo liliokolewa na mlinzi wa sheria mchungaji Christopher Mtikila,ambaye alivamia hapo na kuvunja uzio wa mabati.

 je sasa ni nani atanusulu eneo hilo la kidongo chekundu ambalo licha ya michezo huwa linatumika katika amikutano ya hadhara, Meya Silaa ametamka kwamba kwasasa wanatafuta mwekezaji ajenge maegesho ya magari kwa faida ya Manispaa sio watu wake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages