MACHI 19, 2013 Dar es
Salaam – Wakati umewadia tena wa kushuhudia
mapambano katika kipindi ukipendacho cha Televisheni na kinachotambulika kama, “The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™”, ambacho
kinarudi kwenye runinga yako wiki hiii
tarehe 20 mwezi huu wa tatu.
Mwaka
huu watazamaji watapata nafasi ya kuangalia mchuano huu wa kipindi hiki katika
televisheni mbili ikiwemo televisheni ya
ITV na Clouds TV ambazo zitarusha kipindi hiki kwa muda tofauti tofauti siku
hiyo ya Jumatano.
Ikumbukwe kwamba mamia ya vijana kutoka kona mbali mbali nchini
walichuana vikali hapo leaders club
ambapo walikua na nafasi ya kuweza kuingia kwenye shindano ambalo
lingewawezesha kujishidia kitita cha dola za kimarekani $250,000. Kipindi hiki cha televisheni kinachotazamwa
na wengi barani Afrika kimerudi tena kwa kishindo na kwa sasa kitakuwa
kinashirikisha nchi za barani Africa. Washiriki watakuwa kutoka nchi za Cameroun,
Ghana, Kenya, Tanzania and Uganda na washindi wa mwisho kabisa watajipatia tuzo
ya ‘Pan-African champions.’
Washiriki
wote watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kwamba wanaweza
kuwakilisha nchi zao ipasavyo . GUINNESS ilipigania kutafuta kwa hali ya juu washiriki
walio na uwezo mkubwa na waliokuwa tayari kuonyesha vipaji vyao na ujasiri
kwenye mchezo wa soka. Timu zote zitashiriki
kwa vipaji na kwa uelewa wa soka yaani kwa kiingereza, ‘Skill and Knowledge’ . Kwa hivyo kila timu ina washiriki
wawili. Mmoja kwa maswala ya uelewa na
mwingine kwa suala zima la kipaji.
Kwa kuanza kabisa, watanzania
waliofuzu kusafiri watakutanishwa wenyewe kwa wenyewe jukwaani, na kupewa
maswali na nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye soka. Baada ya hapo watakaothibitisha kuwa wapo juu
zaidi kwa asilimia mia, watapata nafasi ya kuingia kwenye shindano lenyewe
wakipewa dhamana ya kubeba bendera ya nchi yao. Wengine watarudi nyumbani.
Usikose
kipindi cha kwanza kabisa ambacho kitarushwa hewani na televisheni ya ITV saa
tatu na dakika kumi na tano usiku na Clouds TV
saa mbili na dakika kumi na tano usiku siku ya jumatano
tarehe 20 machi mwaka huu. Katika
kipindi hiki, tutapata nafasi ya kushuhudia timu yetu ikichuana vikali katika raundi ya kwanza.
Timu kwenye raundi ya kwanza :
Timu ya bluu – Tanzania:
·
Kutoka Dar es Salaam, Daniel
Msekwa, ndiye kiongozi kwenye maswala ya
maswali yanayohusiana na soka, Mwalimu Akida
Hamad, naye ataonyesha kipaji kwa kucheza .
Daniel ni mfanyakazi wa shirika la bandari Tanzania yaani TPA na Mwalimu
bado ni mwanafunzi wa chuo cha elimu ya juu.
Wote wanakubali kwamba mchezo huu umewapa nafasi vijana wengi kuonyesha
vipaji vyao na kwamba unainua soka sio kwa kucheza tu bali na kuwa na uelewa
kuhusu mchezo mwenyewe. Je wataweza kuendelea
kwenye hatua ya pili?
Timu Nyekundu – Kenya:
·
Hawa wapenzi wa michezo
mmoja ni Michael Kirwa, na mwenzake ni
mwalimu wa mazoezi yaani ‘fitness
trainer’ Stephen Githinji, wote wa jiji la Nairobi. Michael yupo hapa kwa maswala ya kujibu
maswali yani uelewa wa soka naye Stephen ndiye atakayeonyesha vipaji kwa
kucheza .
Timu ya kijani – Uganda:
·
Oscar Boban na Kennedy Andindu, wanatokea kampala na ndio
watakaoakilisha Uganda katika hiki kipindi cha kwanza. Oscar ni mfanyabiashara na ndiye atakayekuwa
mshiriki wa uelewa na kennedy ambaye ni mpenzi wa Arsenal .Yeye atakuwa jukwaani
kuonyesha kipaji chake.
Timu Nyeusi – Kenya:
·
Daniel Muthendu, ni
mhasibu na amekili ni mpenzi mkubwa wa soka na kujiamini kuchuana kwenye
maswali yote yanayohusu mpira huu wa miguu.
Mwenzake ni Oscar Litonde, ambaye ni mchezaji wa mpira, mechi za kirafiki
jijini Nairobi. Hawa nao pia watachuana
vikali na timu tajwa hapo juu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football
challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa
kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya
hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika
tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu
ya mkononi na kompyuta zao.
Pia
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook page www.facebook.com/guinnesskenya
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri,
unatakiwa kuupenda ukurasa huu yaani ‘like’ na utakuwa unapata habari zote kama
zinavyotiririka.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa
ya Endemol iliyopo Afrika Kusini.
Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako.
Usisahau kuwa na
kinywaji chako ukipendacho cha Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na
nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)