SHEREHE za kumtawaza kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis I, zimefanyika katika viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli zake za Papa.
Mapema, Papa Francis alizunguka katika viunga hivyo akiwa katika gari la wazi, akiteremka kuwabariki mahujaji waliofika hapo.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amewataka viongozi na watu wote duniani kuwalinda wanyonge na watu maskini. Watu wapatao 200,000 wamehudhuria sherehe hizo.
Papa Francis alichaguliwa na mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo Februari 28, mwaka huu.
HABARI: BBCSWAHILI, PICHA : AP, REUTERS NA EPA





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)