…………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa
Stars), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP Mazembe ya
DRC wamewasili Jumatatu jioni na kujiunga na wachezaji wenzao tayari kwa
maandalizi ya kuikabili Morocco katika mechi ya kuwania kucheza Fainali
za Kombe la Dunia mwakani.
Wachezaji hao, ambao ni tegemeo
kubwa katika TP Mazembe wamewahakikishia watanzania ushindi Jumapili hii
na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao ya Taifa.
Samatta na Ulimwengu wamewasili nchini wakitokea Nchini Boswana walikokuwa na Timu yao ya TP Mazembe. Akizungumza mara baada ya
kuwasili, Samata alisema ushindi dhidi ya Morocco ni lazima, hivyo
Watanzania wasiwe na hofu na timu yao na wao wako tayari kuliongoza
jahazi hilo la ushindi.
“Tumekuja kuungana na wachezaji
wenzetu wa Timu ya Taifa, tumekuja kuhakikisha timu yetu inashinda na
tuna kila sababu ya kushinda maana tunacheza nyumbani,” alisema Samatta
ambaye aliifungia Tanzania bao la ushindi dhidi ya Cameroon mapema mwaka
huu.
Alisema kuwa wao wako fiti na
hawana tatizo lolote na wanajiunga na kambi usiku huo huo waliowasili na
kuanza mazoezi kama ratiba ilivyo pangwa na hivyo watanzania wajiandae
kushangilia ushindi.
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro lager, imeingia kambini
tangu Jumamosi ilitarajiwa kuanza mazoezi jana Jumanne baada ya
wachezaji wote 23 walioitwa kuripoti kambini.
Kocha wa timu ya Taifa, Kim
Poulsen amekwishasema kuwa hana wasiwasi na Morocco kwani ameshawasoma
na kuona mchezo wao wakati wa Kombe la Afrika na juzi wakati Morocco
ilicheza na Mali kwa hivyo anajua namna ya kuwaandaa wachezaji wake
kukabiliana nao.
Taifa Stars iko katika kundi moja
na Ivory Coast, Morocco na Gambia huku Ivory Coast ikiongoza kwa pointi
nne, Tanzania ya pili na pointi tatu, Morocco pointi mbili na Gambia
pointi moja.
Ushindi katika mechi hii itawapa wachezaji na Watanzania ari ya kusonga mbele zaidi





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)