Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kulia) akizungumza na Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano
wa Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming
(kushoto) baada ya kuwasili leo Machi 11, 2013 kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Guangzhu, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku kumi nchini
China. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai).Picha na Bashir Nkoromo
--
Na Bashir Nkromo-China
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewasili leo Machi 11, 2013
nchini China kuanza ziara ya kikazi ya siku kumi, kwa mwaliko wa Chama
Cha Kikomunisti cha China.
Kinana ambaye ni ziara yake ya kwanza kufanya nchi za nje tangu
ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa C CCM, Oktoba mwaka jana, amewasili
akiambatana na ujumbe wa watu 14 wakiwemo viongozi na maofisa wa Chama
na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, na Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa
Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming.
Katibu Mkuu ambaye aliwasili saa 8 mchana kwa saa za China (sawa na
saa nne asubuhi) za Tanzania, ameambataba na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud,
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro,
Katibu wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Khamis Suleiman Dadi, Katibu wa UWT
Amina Makilangi, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Wenyeviti wa
CCM wa mikoa, Jesca Msambalavangu (Iringa), Maganga Sengerema na Titus
Kamani (Simiyu) na maofisa wa Chama.
Akizungumza kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, Wang alisema, Chama
Cha Kikomunisti cha China kimefarijika na kuona fahari kubwa kwa
kuupokea ugeni wa Kinana, kwa sababu Katibu huyo wa CCM pamoja na kuwa
ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM, pia
ni kiongozi wa kwanza kutembelea China tangu kupatikana kwa uongozi mpya
wa China wa Rais Xi Jimping ambaye pia ndiye Katibu Mkuu wa CPC.
Alisema, China bado inaona umuhimu mkubwa wa kushirikiana na Tanzania
katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu kuinua uchumi kwa ajili ya
kuboresha maisha ya wananchi wa pande mbili za Tanzania na nchi yake.
Wang alisema, kutokana na umuhimu wa ziara hiyo, uongozi wa juu wa
CPC umeandaa ratiba itakayomwezesha Kinana na ujumbe wake kushuhudia
mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali za Uchumi na
namna China chini ya uongozi wa CPC ilivyofanya jitihada hadi kupiga
mapinduzi makubwa ya kiuchumi duniani.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alishukuru kwa
mapokezi makubwa waliyotoa viongozi wa CPC, na kusema kueleza
matumaini yake kwamba CCM itakuwa na mengi ya kujifunza na viongozi hao
kuondoka nayo kwa ajili ya kwenda kuboresha na kuinua zaidi maendeleo ya
Tanzania kiuchumi.
"Tunatambua ninyi (China) mmekuwa washirika wetu wazuri na Tanzania
tangu miaka mingi, kwa mfano mmehusika sana katika ujenzi wa Reli ya
TAZARA ambayo inatoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa, na pia
mmeshiriki kuanzisha viwanda nchini kwentu kikiwemo kiwanda cha Urafiki
pale Ubungo na bado mnaendelea kuwa washirikia wazuri hadi sasa, kwa
kweli tunafurahia sana ushirikiano huu", alisema Kinana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)