Godfrey Mwanansao Afisa Mipango
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi akitoa maelezo ya ubunifu wa kinyago
kinachoonyesha baadhi ya michezo kwa kinamama kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akikagua mabanda ya wadau wa siku ya
wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa Wilayani Nkasi tarehe 08.03.2013.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Kimanta.
Meneja wa PSI Mkoani Rukwa Issa Ismail
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya juu
kazi za shirika hilo Mkoani Rukwa na katika maonyesho hayo. Kulia kwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta, Afisa
Habari Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ramadhan Juma, Mbunge wa
Nkasi Kaskazini CCM Ali Kesi na Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Jakob
Mwaruanda.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Samson
Mashalla akijionea baadhi ya bidhaa zilizokuwa zikionyeshwa na kuuzwa
katika mabanda hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya akizungumza na wananchi katika viwanja vya sabasaba Mjini
Namanyere katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwishoni mwa
juma.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya akizungumza na wananchi Wilayani Nkasi katika maadhimisho ya
siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika Wilayani humo kimkoa tarehe
08.03.2013. Aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kujikwamua
kiuchumi kwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali na kujiunga
kwenye vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo, aliwataka pia
kuzingatia uzazi wa mpango katika kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta
akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Nkasi katika maadhimisho ya siku ya
wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya akizungumza na wananchi wa Kata ya Wampembe kujibu kero zao
alipotembelea kata hiyo tarehe 09.03.2013. Moja ya kero kubwa za
wananchi wa kata hiyo wapatao alfu kumi na tisa (19,000) ni ukosefu wa
huduma muhimu ya mawasiliano ya simu za aina zote, umeme, barabara, na
Zahanati katika vijiji viwili vya kata hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya akiangalia daraja la muda lililoharibika katika kijiji cha
Ng'unde Kata ya Wampembe Wilayani Nkasi tarehe 10.03.2013 alipotembelea
Kata hiyo kuzungumza na wananchi kujua kero zao. Alimuagiza Mkurugenzi
wa Wilaya ya Nkasi kwa kushirikiana na wananchi kujenga daraja hilo
katika kiwango kinachostahiki. Picha na Hamza Temba wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Rukwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)