Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala,
akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup naodha wa
timu ya Jambo Leo, Said Mwishehe, baada ya timu hiyo kuifunga Changamoto
bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja
wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala,
akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup naodha wa
timu ya Business Times 'Business Queens', Lulu Habibu, baada ya timu
hiyo kuifunga TBC jumla ya mabao 39-18 katika mchezo wa fainali
uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es
Salaam.
Mshambuliaji
wa Jambo Leo, Julius Kihampa, akichuana kuwania mpira na beki wa
Changamoto, Emmanuel Balele, wakati wa mchezo huo wa Fainali uliochezwa
leo asubuhi kwenye Uwanja wa Tcc Chang'ombe. Katika mchezo huo Jambo Leo
imeibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutangazwa kutwaa kombe hilo la NSSF
CUP 2013 na kuwa bingwa mpya wa michuano hiyo iliyomalizika leo.
Beki wa Jambo Leo, Mohamed Akida, akimdhibiti kiungo mshambuliaji wa Changamoto, Hamad Ganichiaga, wakati wa mchezo huo.
Beki wa Jambo Leo, Mohamed Akida, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
Kiungo
Mshambuliaji wa Changamoto, Hamad Ganichiaga (kulia) akijaribu kumtoka
beki wa Jambo Leo, Mansour Mohamed, wakati wa mchezo huo.
Beki
wa Jambo Leo, Mansour Mohamed (kushoto) akimdhibiti Kiungo Mshambuliaji
wa Changamoto, Hamad Ganichiaga, wakati wa mchezo huo.
Beki
wa Changamoto, Emmanuel Ganichiaga, akichuana kuwania mpira na
mshambuliaji wa Jambo Leo, Zahor Milanzi, wakati wa mchezo huo.
Kipa wa Jambo Leo, akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Julius Kihampa (chini) akicheza takorling....
Kina Dada wa Jambo Leo, wakiwahamasisha kaka zao.
Benchi la Ufundi la Changamoto na wachezaji wa akiba.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wengine.
Benchi la Jambo Leo.Picha Kwa Hisani Ya Sufianimafoto Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)