Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania, Mhe. Sospeter
Mhongo, akiwa Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe.
Peter Kallaghe, akiangalia Kitabu cha wageni kilichopo Ofisini hapo,
kabla ya kusaini Kitabu hiko.
Mheshimiwa Waziri Sospeter Mhongo (kulia) akiongea
na baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji mapema leo kwenye Mkutano
wake ambao aliufanya kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London,
(kulia),Mhe. Balozi Peter Kallaghe, akisikiliza kwa makini maelezo
kutoka kwa Mhe. Waziri, alipokuwa akiongea na Wawekezaji hao wenye nia
ya kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta hiyo ya Nishati na Madini.
Mheshimiwa Waziri, akibadilishana mawazo na
Wawakilishi kutoka Kampuni ya Margin Capital ya Uingereza, mara baada ya
kumalizika mkutano na Wafanyabiashara na Wawekezaji hao.
Mheshimiwa Waziri Sospeter Mhongo
(kati), akiwa kwenye picha ya pamoja Wawekezaji, (kushoto) Bwana Manubai
Teraiya, mwakilishi wa Lloyds Eastern Group na (kushoto) ni Dada
Gillian Raini Mwakilishi wa Kampuni ya East Africa Ventures
---
WAZIRI
WA NISHATI NA MADINI, MHE. PROF. SOSPETER MUHONGO (MB), KUKUTANA
NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA KESHO, JUMANNE ( 26 FEBRUARI
2013)
Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo, yuko nchini Uingereza kwa
ziara ya kikazi. Leo Jumatatu Tarehe 25 Februari 2013, Mhe. Waziri amekutana
na baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye
Sekta ya Nishati na Madini nchini Tanzania.
Mhe. Waziri Sospeter, alielezea hali halisi ya Uchumi
iliyopo nchini, hususan kwenye sekta ya Nishati na Madini. Aidha alielezea
fursa zilizopo kwa Wawekezaji wa kigeni na Wajasiliamali wa Kitanzania
kuja kuwekeza nchini, ili kulipatia taifa maendeleo ya kiuchumi na kufungua
ajira kwa Watanzania.
Kesho Jumanne tarehe 26 Februari 2013, Mheshimiwa
Waziri anatarajiwa kukutana na Watanzania waishio Uingereza kuzungumzia
maendeleo ya sekta ya nishati na madini Tanzania na pia kubadilishana
nao mawazo kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.
Ubalozi wa Tanzania, London unapenda kuwakaribisha
watanzania wote katika Mkutano huo utakaofanyika Ubalozini (3 Stratford
Place, London W1C 1AS) kuanzia saa 11 Jioni. (17.00PM)
Karibuni sana
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)