Bondia Joseph Agbeko baada ya moja ya ushindi wake
Waghana Frederick Lawson na Issac Sowah wanatarajia kupanda ulingoni tarehe 8 Machi kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Welterwweight kwenye uwanja wa Accra Sports jijini Accra, Ghana.
Mabondia hao wamepangwa katika kapambanoi ya utangukizi wakati wa
mpambano mkubwa wa kugombea mkanda wa dunia kati ya bondia wa Ghana na
ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa bantam Joseph Abgbeko na bondia Luis Melendezkutoka nchi ya Columbia iliyoko bara la Amerika ya Kusini.
IBF inaipa pongezi sana nchi ya Ghana iliyokuwa inaitwa Pwani ya Dhahabu au Gold Coast kwa kuonyesha nia thabiti ya kuinua vipaji vya mchezo wa ngumi na kuufanya mchezo huu kurudi nyumbani. Ghana inasikfika sana kwa kuweza kutoa mabingwa wengi wa nguni wa zamani ambao walisifika sana kwa uwezo wao wa kurusha masumbi wakiwamo D.K. Poison, Marvelous Nana Yaw Konadu, Azumah Nelson, Ike "Bazooka" Quartey, Alfred "Cobra" Kotey na Joseph King Kong Agbeko ambaye anatarajia kuonyesha makeke yake siku hiyo ya tarehe 8 Machi.
Wawili
hao wanatoka katika maskani ya Bukom iliyoko kwenye kiunga cha Lebanon
jijini Accra kinachosifika kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia. Kuingia
kwa mabondia hawa wawili kwenye mpambano huo kutatoa burdani ya aina
yake kwa mashabiki wa ngumi wa Ghana pamoja na nchi nyingi za Afrika ya
Magharibi.
IBF inaipa pongezi sana nchi ya Ghana iliyokuwa inaitwa Pwani ya Dhahabu au Gold Coast kwa kuonyesha nia thabiti ya kuinua vipaji vya mchezo wa ngumi na kuufanya mchezo huu kurudi nyumbani. Ghana inasikfika sana kwa kuweza kutoa mabingwa wengi wa nguni wa zamani ambao walisifika sana kwa uwezo wao wa kurusha masumbi wakiwamo D.K. Poison, Marvelous Nana Yaw Konadu, Azumah Nelson, Ike "Bazooka" Quartey, Alfred "Cobra" Kotey na Joseph King Kong Agbeko ambaye anatarajia kuonyesha makeke yake siku hiyo ya tarehe 8 Machi.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)