RAISI KIKWETE AZINDUA RASMI BARABARA YA MWAI KIBAKI LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

RAISI KIKWETE AZINDUA RASMI BARABARA YA MWAI KIBAKI LEO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakiongozwa na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph  Mwenda kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. Barabara hiyo, yenye urefu wa kilomita 10.1 inaanzia makutano ya barabara za Rashid Kawawa na Bagamoyo hadi njia panda ya kwenda Africana karibu na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ Mbezi Beach
 Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
Vifijo na nderemo baada ya uzinduzi huo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo rasmi(official talks)Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha kwa rais Mwai Kibaki baadhi ya Mawaziri waliohudhuria dhifa ya kitaifa ikulu jinni Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa Ikulu kwa heshima ya Rais Kibaki aliyeko nchini kwa ziara yaka ya mwisho ya kiserikali.Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages