kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara

 Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Mh. Wilman Kapenjama Ndile (kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara leo,tayari kwa ufunguzi wa Kongamano hilo ambalo ni la siku mbili.
Mwenyekiti wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),John Bwire akitoa utambuliwa wa Wanahabari waliohudhulia kongamano hilo toka sehemu mbali mbali hapa nchini,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akitoa taarifa fupi ya Mfuko wa Bima ya Afya kutokana tafiti mbali mbali zilizofanywa na baadhi ya Wanahabari katika Halmashauri 26 hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari hapa nchini,Nevile Meena akizungumza machache wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,linaloendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Raphael Mwamotto akitoa muongozo na utambulisho kwa baadhi ya viongozi kutoka sehemu mbali mbali wanaohudhulia Kongamano hilo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mikongoti akiwasilisha mada yake kwenye Kongamano la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Wadau wakifatilia Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo.
Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Na Othman Michuzi wa www.othmanmichuzi.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages