Mradi wa “Airtel shule yetu” kuleta ufanisi katika masomo ya Sayansi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Mradi wa “Airtel shule yetu” kuleta ufanisi katika masomo ya Sayansi


 Meneja huduma kwa  wateja wa Airtel Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza  Hamisi Maulidi msaada wa vitabu kwa shule tatu za sekondari za Kalebezo, Buhongwa, and Kabuhoro zilizopo mkoani Mwanza. wakishuhudia kulia ni  Meneja Mauzo wa Kanda Ally Maswanya na Meneja huduma ya Airtel money wa  Kanda Galus Mgawe.

Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulidi  akipokea msaada wa vitabu  kutoka kwa Meneja huduma kwa wateja wa Airtel Hawa Bayumi  zilivyokabithiwa  na Airtel chini ya mradi wake wa Shule yetu, shule 3  za sekondari za  Kalebezo, Buhongwa na  Kabuhoro za mkoani Mwanza  zilifaidika na Msaada huo.
 =======  ======= ====== 
Mradi wa “Airtel shule yetu” kuleta ufanisi katika masomo ya Sayansi
Airtel yachangi vitabu vya sayansi kwa shule 3 za sekondari mkoani Mwanza

Wakati Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa fani ya sayansi,wanafunzi wametakiwa kutohofia masomo ya sayansi na kukimbilia kusoma masomo  mengine kwa lengo la kulifanya taifa liwe na wataalamu wengi wa fani  mbalimbali.Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Afisa Elimu wa Mkoa wa  Mwanza Hamis Maulid wakati akikabidhi vitabu kwa shule nne za sekondari  za mkoa huo vilivyotelewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Afisa Elimu wa mkoa wa mwanza ameendelea kwa kusema elimu ni urithi endelevu  na kusoma masomo ya sayansi kunamwezesha mwanafunzi kuwa katika nafasi  nzuri ya kulisaidia taifa katika Nyanja ya kitaalamu. mataifa mengi  duniani yamepiga hatua kutokana na wanafunzi kupewa msukumo wa kusoma  masomo ya mchepuo wa sayansi.
Akiongea katika halfa ya makabithiano ya vitabu mkoani Mwanza, Meneja wa huduma  kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Hawa Bayumi amesema  Airtel imeguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni na kusababisha  kiwango cha ufaulu kushuka hasa katika masomo ya sayansi. Na leo  tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari  za mkoa wa  mwanza zikiwemo: Kalebezo  sekondari iliyopo wilayani Sengerema, shule  ya sekondari ya Buhongwa na Kabuhoro sekondari.
Tunaamini mchango huu wa vitabu mashule utakuwa chachu ya maendeleo ya elimu  nchini na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini. Tunaahidi kuendelea  kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha  tunafikia malengo waliojiwekea. Aliongeza Bayumi.
 Naye Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kalebezo iliyopo wilayani  Sengerema Thomas Muswaga na mwanafuzi Julieth John wa kidato cha nne  katika shule ya sekondari ya Buhongwa wanazungumzia changamoto  mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu na kushukuru Airtel kwa msaada wa  vitabu walioutoa katika shule hizo za mkoa wa Mwanza

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages