RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AFUNGUA KATUO CHA KURUSHIA MATANGAZO YA DIJITALI ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AFUNGUA KATUO CHA KURUSHIA MATANGAZO YA DIJITALI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akikata Utepe kuonyesha Ufunguzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia Matangazo ya Dijitall huko Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kituo kikuu cha Mtambo wa Kurushia Matangazo ya Dijitall kilichofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi huko Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akipata maelezo mafupi kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Agape Association LTD Dr Vernon Fernandes wakwanza kuli kuhusiana na Chanall za Dijitall zinavyofanya kazi,baada ya Rais kufungua Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo Mjini Zanzibar.wapili kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Mainjinia wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo Mjini Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar   

 SHIRIKA la Utangazaji  Zanzibar ZBC limetakiwa kuhakikisha kwamba linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa kulingana na mfumo uliopo hivi sasa.
Alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wameonakana wakifanya kazi kimazowea tu bila kufuata taratibu za kikazi.  

Hayo yameelezwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt Ali Mohammed Shein katika Uzinduzi wa Miundombinu ya Dijitali na Jengo la Studio ya Kisasa Alisema kuwa kubadilika kwa watendaji kazi ni suala la lazima kutokana na mabadiliko makubwa yalioko duniani .

Dkt Shein alisema kuwa ZBC wananchi wengi wanapiga kelele juu ya utendaji wa wafanyakazi wa ZBC kutokana na  vipindi vyao kutoridhisha na kukatika katika kwa matangazo yao zaidi wakati wa taarifa ya habari.

Alisema kuwa Zanzibar inaheshima yakekatika masuala ya Utangazaji kwani Redio nyingi za Nje zinawatangazaji kutoka Zanzibar ambao ni mahiri katika masuala ya Utangazaji.


Dkt Shein amesema kuwa hivi sasa hatoweza kuvumilia tena kutokana na utendajihuo ambao hauridhishi hata kidogo na hasa sasa tulivyoingia katika mfumo huu wa DIGITALI. “Sitaki kuiona Serikali ambayo nnayoiongoza mie iwe ‘tiro’(mwisho) alisema Dkt Shein.
 
Alisema kuwa kuingia katika mfumo mpya wa dijitali ni kazi kubwa lazima watendaji wafanyekazi kwa mashirikiano na kuwe na uwiano baina yao ili kuweze kuwa na kiwango ambacho kitaweza kuwajengea sifa wafanyakazi hao.

Alieleza kuwa madhumuni makubwa ya Mapinduzi ni kuweza kuwakomboa wanyonge na  kuwabadilisha maisha yao sitofurahishwa na kuona gharama zote zilizotumika katika kuingia katika mfumo huo mpya wa Digitali kuweza kupotea bure lazima viongozi waweze kusimamia majukumu yao na kuanzia hivi sasa lazima mambo yende.
‘’Hakuna aliekamilika lakini tujitahidi’’ alisema Dkt Shein .

Dkt Shein alimtaka Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk pamoja na Katibu wake kuisimamia ipasavyo Shirika hilo la ZBC na kuhakikishakuwa mambo yanakwenda vizuri.

Akizungumzia  juu ya Studio ya Kurikodia Dkt Shein amesema kuwa  madhumuni ya kutengeneza Studio hiyo ni kwaajili ya Wasanii wa Zanzibar waweze kupata nafasi nzuri za kurekodia nyimbo zao na hapo hapo kuwa na pahala ambapo wataweza kurekodi michezo ya kuigiza napia kuonesha maigizo mbali mbali katika ukumbi huo.

Nae Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema kuwa  miundombinu  mipya ya Digitali ni mkataba baina ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni ya Ágape na imeagharimu jumla ya Shs billion 8  za Tanzania na kuweza kujengea vituo 6 vya kurushia matangazo vikiwamo vya Kizimkazi, Nungwi na Masingini.  Kwa upande wa Pemba ni Konde,Mizimiumbi  na Mkanjuni.

Aidha alisema kuwa ifikapo tarehe 28 /2/ 2013 analogi itazimwa na kuanza mfumo mpya wa dijitali na kuwaeleza wananchi wasiwe na wasiwasi ya upataji wa vingamuzi ambavyo vitakuwa vyakisasa na madhubuti.

Said  alisemakuwa vingamuzi hivyo vitapatikana kwa katika sehemu mbali mbali  za Wilaya zote kumi za Zanzibar na hakutakuwa na haja kwa watu kufuatia Mijini.

Alisema kuwa kila kingamuzi kimoja kinatarajiwa kuuzwa si zaidi ya shs za Tanzania 50,000 na malipo ya matangazo yatakuwa si zaidi ya shiling za Tanzania 8000 vikiwa na chanal 36-38.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages