Bibi shamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akipokea zawadi
ya sh. 305,000/- kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambazo
zilichangwa papo hapo na watu alioandamana nao ili kumpongeza kwa kazi
nzuri aliyoifanya kwenye shamba darasa. Wa pili kulia ni Bw. Joseph
Laurent anayesimamiwa na bibishamba huyo ambaye shamba lake lilikaguliwa
na Waziri Mkuu katika kijiji cha Itenka juzi jioni (Januari 6, 2013)
wilayani Mlele, Katavi. Pia aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie
kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitaka maelezo zaidi kuhusu aina ya
mbegu ya mahindi iliyotumika kutoka kwa Bi. Grace Hokororo ambaye ni
Bibishamba wa kata ya Itenka wakati alipokuwa akikagua shamba darasa
analolisimamia kwenye kijiji cha Itenka wilayani Mlele, Katavi, juzi
jioni (Januari 6, 2013). Alifurahia kazi yake na kuahidi kumpatia
pikipiki imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)